Nifanyaje jamani !

mkolaj

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
3,023
Reaction score
1,092
Jamani wana MMU habari zenu,

Waungwana naomba ushauri wenu kwani mimi nimetokewa kupendwa na dada mmoja ambae anasomea nursing na atakua anahitimu mwezi wa sita na amekuwa akiambia anataka aolewe nami, pia anasema kuwa kwa hali yoyote ile lazima atafanya ili kuhakikisha namuoa, kiukweli hata mimi nampenda sana huyu mwanamke ila tatizo ni kwamba nina mke tayari ambae nimemuoa na tumebahatika kuwa mtoto mmoja wa kiume na bado nampenda mke wangu. Dini yangu inaruhusu kuwa na wanawake wa ndoa zaidi ya mmoja, isitoshe huyu mwanamke namuambia kuwa nimeoa ila adai yeye yuko tayari hata wakiwa wawili lakini mimi kwa upande wangu siko tayari kuwa na wanawake zaidi ya mmoja. Naombeni ushauri nifanyaje?
 
Mwambie huwezi kumuoa,ijapokuwa dini inaruhusu na ameridhia kuwa mke mwenza lakini huwezi mikiki ya mke zaidi ya mmoja ….
 

Mie hapo ndo nkapata swali "dini yako inakuruhusu kuzini na kumcheat mkeo?" Mana mie sijaelewa msaada unaotaka hapo ni wanini sasa au unataka tukwambie mwache mkeo umuoe huyo unayempenda nw au?

Happy Holly Week
 
Komaa na msimamo wako. Itakuwa unamwambia kwa utani utani ndo mana anakwambia hivyo.

Je huwa unamgegeda na ukimgegeda unakuwa unampa ahadi gani?
 
ng'oa macho yako yatupe

unataka tukushaurije? kuwa umuache mkeo?

hebua ach tamaa,

kama unaona dini inaruhusu oa

kama hutaki mke zaidi ya mmoja mwambie huyo mwanamke hutaki

mbona huna msimamo mwanaume????????????
 
Mwambie huwezi kuwa na wake wawili, ila unaweza kuwa na mke mmoja na mchepuko mmoja, Kama atakubali kuwa mchepuko hapo haina tatizo.

Ushauri mzuri maana kuwa na wake wawili hawezi ila anaweza kuwa na mke anayempenda sana na mchepuko anayempenda sana
 
Weee tayari hutaki wake wawili then wataka ushauri wabongo bana ndo mana hatupati katiba ya wananchi .... Samahan lakin ;

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
muone huyu nae, hivi unajua nini maana ya mke na sio mpenzi, u how, hakuna ushauri wa kutenganisha ndoa hapa, utajua utakavyodil na huyo ndogo mtarajiwa
 
Mwambie ukweli vile unavyojisikia, ingawa itachukua muda lakini atakuelewa

Ila nashindwa kukuelewa unavyosema unampenda sana mchepuko na unampenda pia mkeo inaelekea kuna mmoja lazidi atazidi upendo sababu upendo hauwezi kuwa sawa hata siku moja, kwa vile umeshaoa ningekushauri ubaki na mkeo na uachane na mchepuko ili aangalie ustaarabu wake isije kuwa unamzibia riziki kwa wengine ambao watakuwa tayari kumuoa.
 

kamwambie mkeo yote uliyoyaandika hapa ndo atakushauri vizuri cha kufanya
 
Sasa unaomba ushauri wa nini wakati ushasema huwezi kuwa na wanawake wawili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…