NIDA Tafadhari.

Kuhara

Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
47
Reaction score
43
NIDA Kuna Jambo linaendelea katika simu za Wananchi ambao Hawajasajiliwa na hata kujiandikisha ili Wapate Namba Ya Uraia Wa Tanzania, Nalo ni Wanapokea Ujumbe Wenye namba za Uraia tokea NIDA na wanafurahia kufikiria Mumeamua kuzigawa kwa Mtindo huo Pasipo jiandikisha ama lah na Mwisho wa siku Wakienda kusajiri wanajibiwa Umetumiwa kimakosa Namba ni Ya mtu Mwingine.

Sawa ila imekaaje hapo Tafadhari Kiusalama Namba ya Uwesu kutumiwa Chijinga?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Voda wameniambia nikajisajili watanipa bando la GB moja hapo sawa, kesho nitaenda
 
Kama ulijiandikisha sawa hiyo inaeleweka, lakini hukujiandikisha halafu utake kuitumia kusajili line?
 
Nchi ya hovyo hii

Mimi nahoji Kwani tunawahi wapi na huu usajili wa Fingerprint ??
Yani ni hovyo hovyo
Sasa ona kama hapo watu wanapewa Namba pengine Hata form hajajaza
 
NIDA n janga la kitaifa,yaan mtu unenda kujaza fomu halafu wanakwambia njoo kesho,kesho ukienda wakwambia fomu hazipo,ctak hata kuwasikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…