Akihojiwa katika kipindi cha asubuhi hii kinachorushwa na TBC-Taifa katibu mkuu wa TUCTA, Bw .Nicholaus Mgaya amesema katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru, watumishi wa umma wanasherehekea wakiwa na hali duni kimaslahi. Mishahara pamoja na marupurupu bado ni duni na hivyo kusababisha baadhi yao kujiingiza kwenye masuala ya rushwa. Pia ametamba kuhusu mafanikio ya TUCTA kuwa ni pamoja na kuishinikiza serikali hadi ikaongeza mshahara kwa 29.7 mwaka 2010. Hapa ananichanganya, inakuwaje aseme maslahi duni wakati serikali imeongeza kiasi kikubwa cha mshahara kama hicho? Wadau hii imekaaje!