Nicholaus mgaya anasema kweli kuhusu ustawi wa watumishi?

Brightman Jr

JF-Expert Member
Mar 22, 2009
1,225
232
Akihojiwa katika kipindi cha asubuhi hii kinachorushwa na TBC-Taifa katibu mkuu wa TUCTA, Bw .Nicholaus Mgaya amesema katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru, watumishi wa umma wanasherehekea wakiwa na hali duni kimaslahi. Mishahara pamoja na marupurupu bado ni duni na hivyo kusababisha baadhi yao kujiingiza kwenye masuala ya rushwa. Pia ametamba kuhusu mafanikio ya TUCTA kuwa ni pamoja na kuishinikiza serikali hadi ikaongeza mshahara kwa 29.7 mwaka 2010. Hapa ananichanganya, inakuwaje aseme maslahi duni wakati serikali imeongeza kiasi kikubwa cha mshahara kama hicho? Wadau hii imekaaje!
 
Mbona lipo wazi, ina maana kabla ya hiyo nyongeza ya mishahara ya 29.7% mishahara ilikuwa midogo sana. Lakini licha ya nyongeza hiyo bado mtumishi wa serikali ana hali mbaya kulingana na hali ya sasa. Nadhani alikusudia hivyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom