Serikali iko mbioni kuanzisha na kumalizia ujenzi wa shule ili watoto wetu wapate elimu karibu na maeneo yao badala ya kutembea umbali mrefu kufuata elimu, iko mbioni kujenga hospital ili kuokoa afya zetu na watoto, inajenga barabara ili kurahisishia wakulima waweze kuvuna na kuuza mazao yao kwa wakati, inajenga miundo mbinu ya kurahisisha upatikanaji wa maji na umeme. Haya ndio mambo ya muhimu ambayo watu wanaweza kuyajadili. Sio mambo ya katiba ambayo yatatumiwa na wanasiasa kama uchochoro wa kupiga hela kupitia vikao vya katiba hiyo. Kama chama kinataka katiba kiweke katika ilani yake ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025. Ila kwa sasa hatuwezi kukubali serikali iache yale iliyoahidi kuyafanya kwa wananchi wake eti kwa ajili ya kutengeneza katiba ambayo itakuwa na faida zaidi kwa wanasiasa.