Utafiti wa Twaweza katika ripoti ya Maoni ya wananchi juu ya walemavu; umeonyesha kuwa walipo fanya utafiti wao wa "Sauti za Wananchi" - moja kati ya watu wanane nchini wamesikia juu ya Zeruzeru ambae kapata madhara.
Madhara hayo mara nyingi huwa kudhuriwa ama kuuawa na kuchukuliwa viungo katika miili yao kwa kile kinachoaminika ni sababu za Kishirikina. Suala hili hufanya Zeruzeru wengi kuogopa na kutoishi kwa amani.
Nje ya suala hili, mie naona mtu ambaye ni Zeruzeru hapaswi kuitwa ni Mlemavu, bali kwa jina lingine.
Naamini kuwa Mlemavu ni yule ambaye huwa na kasoro katika viungo vyake vya mwili.
Wadau mna maoni gani?
Nawasilisha.
Hili ni Jedwari number 5: katika utafiti wa Sauti za wananchi likionyesha takwimu za watu waliosikia waathirika Zeruzeru.
Ulemavu ni hali ya upungufu au kushindwa kufanya mambo yanayohesabika kuwa ya kawaida.
Albino ni mlemavu kwasababu kuna mazingira hatoweza ku perform normal unless apate vifaa saidizi kumrahisishia
1. Hawezi kukaa juani kama asiye albino.
2. Ngozi yake iko so delicate kwenye kupata skin cancer na kuathiriwa na mionzi
3. Albino wote wana uoni hafifu(low vision) hivyo ni lazma apate vifaa saidizi kumuwezesha kuishi kawaida ndo mana wanaingia kwenye kundi la walemavu