Ni kweli mshahara Hayati Magufuli ulikuwa 9M?

So JK alikuwa analipwa 9M maana Katiba hairuhusu kupunguza hata kama yeye angetaka.
 
Rais yoyote analipwa 108M kwa mwezi

Anaefuata ni Gavana wa Benki kuu kwa mwezi ni 78M
Sentensi yako ina ukakasi kwamba kuanzia Kina Mwinyi Mkapa, JPM na Huyu wa sasa huwa wanalipwa 108M yaani hazipandi ? au unamaanisha JPM na wa sasa ndio wanavuta hio ?
 
So JK alikuwa analipwa 9M maana Katiba hairuhusu kupunguza hata kama yeye angetaka.
Ndio maana nikasema ile statement ilikuwa na walakini sababu JK it was reported kabla kwamba alikuwa anakula mara tatu ya hizo...

Ila point yangu kubwa zaidi kwa leo sio wanachukua ngapi bali inabidi tujue tunachowalipa sio kusubiri tetesi na dondooo ; Yaani when it comes to watumishi wetu na Mali zetu za UMMA ningependa sana kuwe na UWAZI
 
Sentensi yako ina ukakasi kwamba kuanzia Kina Mwinyi Mkapa, JPM na Huyu wa sasa huwa wanalipwa 108M yaani hazipandi ? au unamaanisha JPM na wa sasa ndio wanavuta hio ?
Haiwezi kuwa figure kubwa hivi huku watumishi wengine wakiwa chini...Mshahara utakuwa huo huo 9M ila marupurupu ndiyo yatakuwa mengi. Mshahara wa mbunge ni 4M chini ya ule wa wanataaluma lakini marupurupu Yao yanafikisha kabla ya kuongeza posho 11.9M
 
Sasa hicho nacho ni kichekesho maana mbona marupurupu ni makubwa kuliko Mshahara wenyewe.

Yani hapo kitaalamu ni sawa na Siku yako ya Birthday uvae Suti/Shela alafu siku yako ya Harusi uvae kaptula na Singlendi.
Watawala wengi wanapitia kwenye hio loophole mishahara midogo lakini marupurupu ni balaa na uzuri marupurupu hayana makato yoyote (in case ya watawala wengine i.e. Wabunge)
 
Unamdai kwani
 
Sentensi yako ina ukakasi kwamba kuanzia Kina Mwinyi Mkapa, JPM na Huyu wa sasa huwa wanalipwa 108M yaani hazipandi ? au unamaanisha JPM na wa sasa ndio wanavuta hio ?

That was by JK time: probably kwa sasa ni zaidi ya hizo

Jiongeze kaka unataka nikuandikie kuwa kila mwezi inapanda au kila Mwaka : Mbona ipo obviously .

Yaani you want things to be written literally

Bwashee namna gani tena
 
Haiwezi kuwa figure kubwa hivi huku watumishi wengine wakiwa chini...Mshahara utakuwa huo huo 9M ila marupurupu ndiyo yatakuwa mengi. Mshahara wa mbunge ni 4M chini ya ule wa wanataaluma lakini marupurupu Yao yanafikisha kabla ya kuongeza posho 11.9M

Hakuna mnachojua Nyie waafrika

Ikiwa MKURUGENZI MKUU wa NIMR , NSSF, NHIF mishahara yao not less than 20M

Na kuna taasisi CEO wao ni 35M on monthly

Unaamini RAIS analipwa 9 M

That was JPM politics
 
Unamdai kwani
Sio mimi tu hata wewe kama mlipa Kodi hizo pesa wanazolipwa ni za kwako na una-stake katika utendaji wao; kama hawafanyi kazi zao basi ni jukumu lako kuwadai..; Unless unadhani bado tupo kwenye Mfumo wa Kifalme
 
Kinadhalia ipo hivyo, lakini mishahara kwao imekuwa kama gelesha tu, kuna watumishi wanalipwa laki 3 hadi 4 lakini maisha na mali wanazomiliki hatari.
 
Million 9 hata mfanya biashara wa kuku wa kizungu mitaani anaipata eti MAGU mshahara wake ndio huo pumbavu sana
 
Million 9 hata mfanya biashara wa kuku wa kizungu mitaani anaipata eti MAGU mshahara wake ndio huo pumbavu sana
Muuza Kuku wa kizungu ni pesa yake na nguvu zake hawa ni sisi ndio tunawalipa hata kama ingekuwa hio kwangu mimi mlipa Kodi bado ni nyingi sana (ukizingatia hapo kuna marupurupu na hatumii hata senti yake moja kufanya chochote) yaani hizo ni kama petty cash

Ila sababu mawazo yetu tunadhani ukiwa Rais ni kama Ufalme ndio maana wanaweza wakajipangia mishahara wanayotaka
 
Hakuna mnachojua Nyie waafrika

Ikiwa MKURUGENZI MKUU wa NIMR , NSSF, NHIF mishahara yao not less than 20M

Na kuna taasisi CEO wao ni 35M on monthly

Unaamini RAIS analipwa 9 M

That was JPM politics
By the way wewe binafsi unaona ni sawa au kuna ulazima wa Rais kuwa Highest Earner kwenye Nchi ?

Ukizingatia nchi ambayo ina matozo ya kila aina kwa watu ambao milo mitatu sio guarantee na wanatembeza bakuli kila kona ? Binafsi hata mcheza karata akilipwa milioni hamsini kwa dakika ni sawa sababu anaingiza hizo pesa na watazamaji wanalipa willingly hili kuona anachofanya (Sasa huku hata walipaji hatujui ni ngapi wala hatuwezi ku-afford kuwalipa hata robo ya hio; ni ombaomba)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…