Hivi ni kwanini nguzo za zege hazitumiki kama nguzo za umeme?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,063
40,724
Je, kuna haja ya kuagiza nguzo kutoka south Africa au kuharibu misitu wakati cement tunayo, kokoto tunazo na mchanga tunao?

=================================

fa3ca0773a42e6ad48e8e2bf9d2d.jpg


electric-Concrete-pole-making-machine-and-moulds.jpg_350x350.jpg

Nguzo hizi zinauwezo wa kudumu kwa muda wa hadi miaka 300 bila kuoza wala kuliwa na mchwa, na ni very light weight kwa sababu ni hollow na technology imekuwa sana ya kuzifanya nyepesi kama mabua ila ngumu kama steel

================================
Update: 05/07/2021
Hongereni DERM ELECTRICS, naona mnakula vinono kiulaini kabisa

===============================
Update: 06/07/2021
Tanesco hawajui kutumia pima maji na biriji, asilimia kubwa ya nguzo wanazosimika zinakuwa zimelala (inclined) na kuharibu kabisa unadhifu wa kazi
 
Kenya zinatumika! barabara ya lamu kutoka mpeketoni mpaka lamu kuna nguzo za zege,sisi tu mpaka tununue za SA
 
hata tz tunazo ila ni kwa uchache nimepata kuziona hivyo ni wazi tunazo ingawa sio kwa wingi kama nchi jirani hasa Kenya zinatumika sanaa sijajua kwanini??
 
Basi Muhongo alione na hili shauri
Muhongo ajitahidi kuvutia wawekezaji, maana Tanesco haina mpinzani katika hii biashara, wao ndio dominant, wawahakikishie investors soko la uhakika la ndani, sio mnakazana kuagiza nguzo toka sa kama mapoyoyo
 
Kenya zinatumika! barabara ya lamu kutoka mpeketoni mpaka lamu kuna nguzo za zege,sisi tu mpaka tununue za SA

Tatizo ni kwamba vitu vibavyotengenezwa hapa Tanzania ni ghali kuliko vinavyotoka nje. Mfano mchele wa malaysia ni rahisi kuliko wa kyela mbeya.

Nasikia tanesco wakitangaza tenda ya nguzo,wazalishaji wa nguzo toka tanzania wanakua na bei kubwa kuliko nguzo zinazotoka nje ya nchi.

Yaani wanaenda sa kununua nguzo na kuzisafirisha hadi hapa bei inakua chinikuliko za kutoka iringa na kujenga mradi wa hap hapo iringa.
 
Je, kuna haja ya kuagiza nguzo kutoka south Africa au kuharibu misitu wakati cement tunayo, kokoto tunazo na mchanga tunao?

Mkuu kitu chochote ambacho ni rahisi mara nyingi ni ghali sana. Unaposema kokoto, cement na misitu ya kukata miti tunayo una maana gani? Je, hizo wanazoagiza kutoka SA kazi yake ni nini? Je, Nani anaagiza? Je, hizo nguzo kazi yake ni nini?
 
Kenya zinatumika! barabara ya lamu kutoka mpeketoni mpaka lamu kuna nguzo za zege,sisi tu mpaka tununue za SA

Wanapotumia Kenya sio lazima na sisi tuige. Zinatumika barabarani kwa shughuli gani? Kubeba umeme kwenda mahali pengine au kwa taa za barabarani?
 
Back
Top Bottom