Nguvu ya mapenzi pengine ni ya pili

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,485
Wadau wa MMU habari zenu! Nyimbo nyingi sana zimeimbwa juu ya hii kitu inayoitwa MAPENZI.Mapenzi yana nguvu kali kama ile nguvu iliyopo kwenye imani za kiroho (DINI).

Ukiyachukulia mapenzi vibaya hakika yanaleta maafa,kama vile dini ikifanyiwa masihara ni maangamizi tu.

Ukifumaniwa na mke au mme wa mtu ni dhahama tu.Ukikashifu dini ya mtu ni dhoruba vilevile.

Angalia yaliyotokea Afrika ya kati baina ya makundi ya Seleka na Ant Baraka.

MAPENZI yakoje? utamkuta mtoto kwao mambo safi maisaha ni full ceremony lakini anakondeshwa ni kijamaa kutoka uswazi tena madongo poromoka,kijamaa hakimpi hela ya shule wala matumizi lakini mtoto haoni hasikii.

Wazazi wengine wakigundua hufanya kazi ya ziada kuwatenganisha na hata kwa vitisho lakini binti wa watu haelewi wala hasikii.

Hii iko na kinyume chake.Nyingine ni hii, mtu hata sio baba yako wala sio mamako ati akikuacha unakonda kwa mawazo ikoje hii.?

Unafahamu kuwa kuna watu huwa wanafeli masomo kwa sababu ya mapenzi?

Je wale ambao wali commit succide kwa ajili ya mapenzi uliwahi kuwasikia?

Unakumbuka kuna watu waliwahi kusambaratishwa viungo na kupotea kabisa katika ramani ya dunia kwa sababu ya mapenzi?

Unajua kuwa kuna watu waliwauwa wenzao kwa kukataliwa tu?

Mapenzi yana vituko vingi katika sayari hii.

Mapenzi ni zaidi ya tuyajuavyo, ni complicated.Nakutajia watu maarufu sana wachache tu, waliowahi kuvurugwa na mapenzi.

Ni kipenzi chetu Mfalme Daudi,Bill Clinton,Nelson Mandela na Princes Diana! Hawa ni wachache sana.

Nawaasa wavulana,wasichana,vijana na wazee kuweni makini sana na hii kitu mapenzi kumbuka kadri siku ziendavyo mbele wanazaliwa watoto wa kiume na kike wazuri wa wazuri,tulieni jamani!.

Kiukweli mapenzi ni matamu sana lakini ni balaa Kubwa,ukijichanganya tu imekula kwako.Mapenzi matamu jama,matamu bwana.

Ukimtia mtu wa dream yako mikononi mwako uta enjoy,lakini siku mapenzi yakigeuka yanakua vita, na uzito wa mapenzi ndio uzito wa chuki,siku mkivurugana.Hakuna ufundi hapa.Amini nakueleza inawezekana mapenzi yakawa ni imani kali ya pili kutoka imani za ki roho.wewe unaonaje?
 
Mapenzi ni namba moja, dini, siasa baadaye.
Yakiharibika yanaharibu kila kitu.
Yakizidishwa balaa.
Yakipunguzwa vilio.
Yasipokuwepo tabu.
Halafu hakuna siku yatakuwa sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…