"Kansa inayoongoza kwa Tanzania ni Kansa ya Shingo ya Kizazi. Kuna baadhi ya Kansa zinasababishwa na kirusi anayeitwa HPV. Kirusi huyu anaambukizwa kwa njia ya ngono kama vile mtu anavyopata HIV. Huyu HPV ameonekana kushirikishwa kwenye Kansa ya Shingo ya Kizazi ambayo inaoongoza hapa Tanzania.