Neumonia inaweza kumbana mtoto ghafla bila dalili?

left eye

JF-Expert Member
Jun 30, 2018
225
301
Mwanang wa pekee amefariki masiku machache yaliyopita kwa kinachosadikiwa ni neumonia

Toka azaliwe alikuwa na afya njema ila ghafla alipoamka asubh saa 3 akanyonya vizuri kidogo. Ghafla akabanwa kifua na kutapika maziwa na kubanwa kifua kwa kasi sana.

Tulimpeleka hospital ya magereza ukonga maarufu KM ila saa zima pale walihangaika kutafuta mshipa wamchome ila walishindwa hapo hal ikazid kuwa mbaya zaid ikabid nimkimbize pugu kufika too late anawekewa oxygen anafariki

Nataka kujuwa kwa wataalamu neumonia inaweza kumbana mtoto ghafla pasina kuwa na dalil zake masiku machache nyuma na kumuua?

Huduma ya kwanza ni ipi? Nimeona inauwa karibia watoto laki 7 kila mwaka dunian. Je, haina chanjo?

Daktari nilipomuuliza nini kimemuua akajibu ni severe neumonia
 
Toka azaliwe alikuwa na afya njema ila ghafla alipoamka asubh saa 3 akanyonya vizur kidogo ..ghafla akabanwa kifua na kutapika maziwa na kubanwa kifua kwa kasi sana ..tulimpeleka hospital ya magereza ukonga maarufu KM ila saa zima pale walihangaika kutafuta mshipa wamchome ila walishindwa hapo hal ikazid kuwa mbaya zaid ikabid nimkimbize pugu kufika too late anawekewa oxygen anafariki

Nataka kujuwa kwa wataalamu neumonia inaweza kumbana mtoto ghafla pasina kuwa na dalil zake masiku machache nyuma na kumuua?? Huduma ya kwanza ni ipi ..nimeona inauwa karibia watoto laki 7 kila mwaka dunian...je haina chanjo ???

Daktar nlipomuuliza nini kimemuua akajib ni severe neumonia
pole sana, mi najua postmortem report ndio inaweza kutoa majibu ya kifo kilitokana na nini. DR Mambo Jambo anaweza kutupa majibu hapa
 
Alikuw nazo mda wote na usiku hakuwa na barid bal kutokana na joto kali lililokuwepo mwez uliopita alikuwa anatoka jasho sana usiku
Haikuwa imeandikwa aendelee na maisha zaidi ya pale, mshukuruni mungu kwa zawadi ya maisha yake japo yalikua mafupi, ila hakuja bure na wala hakuondoka bure, ajaliwe kuwa sehemu yenye furaha ya milele.
 
Kwel kabsa ...siunajuwa hospital zetu hata kupimwa pale pugu hakupimwa wala tulipotoka na alipofariki tu bas ndio ikawa ivo ripot ya dokta ndio ilisema ivo ila hakumpima
Mara nyingi nimeshuhudia wagonjwa wakifa kwa sababu ya uzembe wa watoa huduma halafu mwishoni wanaandika death ripoti nzuri tu ya uongo maisha yanasonga.
 
Mwanang wa pekee amefariki masiku machache yaliyopita kwa kinachosadikiwa ni neumonia

Toka azaliwe alikuwa na afya njema ila ghafla alipoamka asubh saa 3 akanyonya vizuri kidogo. Ghafla akabanwa kifua na kutapika maziwa na kubanwa kifua kwa kasi sana.

Tulimpeleka hospital ya magereza ukonga maarufu KM ila saa zima pale walihangaika kutafuta mshipa wamchome ila walishindwa hapo hal ikazid kuwa mbaya zaid ikabid nimkimbize pugu kufika too late anawekewa oxygen anafariki

Nataka kujuwa kwa wataalamu neumonia inaweza kumbana mtoto ghafla pasina kuwa na dalil zake masiku machache nyuma na kumuua?

Huduma ya kwanza ni ipi? Nimeona inauwa karibia watoto laki 7 kila mwaka dunian. Je, haina chanjo?

Daktari nilipomuuliza nini kimemuua akajibu ni severe neumonia

Pole sana kiongozi kwa msiba! Pneumonia ni bacterial au viral infection na haiji ghafla tena inaambatana na homa na kukohoa sana. Kwa maelezo yako kwa haraka inaweza kuwa ni Aspiration ya maziwa ya kichanga, yani amenyonya na maziwa yakaenda kwenye njia ya hewa badala ya tumboni. Hii mara nyingi inawapata wamama wanaozaa mara ya kwanza endapo hawajafundishwa namna ya kunyonyesha sawasawa. Inatokea kwenye positioning ya namna mtoto anavyowekwa wakati ananyonya au pia ananyonya wkt analia so maziwa yanakosea njia matokeo ya aspiration ni kifo na au huduma za haraka sana za ICU. So kwa namna yyt vituo ulivyotaja havina competence ya kufanya hizo huduma kwa vifaa, tech na staffing unless kungekua na nurse aliyespecialize kuhudumia watoto, wana uwezo wa kusaidia hata kwenye mazingira magumu ya upungufu wa vifaa ambao pia ni wachache sn kwa nchi yetu.
 
pole sana, mi najua postmortem report ndio inaweza kutoa majibu ya kifo kilitokana na nini. DR Mambo Jambo anaweza kutupa majibu hapa
Poleni Sana na hasa left eye Polee sana kaka/Dada..

Ili kuweza Kuwa sawa Anatakiwa kuacha Kujilaumu au Kutojivika Lawama kwa kile kitu ambacho hakukijua kabla sio kosa lake..

Unaweza ukawa umeiona Dalili ya Pneumonia lakini ukashindwa kuijua kwa kuwa hukuwa Mtaalamu wa Afya..

Kingine magonjwa yote huweza kuchukua sura mbili za Ugonjwa kuna namaanisha Huweza h
kutokea Ghafla (Suddenly onset) bila kuonyesha dalili Za hatari na huitwa Acute Diseases na pia Kuna magonjwa Huonyesha Dalili nyingi na huanza taratibu Huitwa Chronic Disease

Hata Pneumonia Huweza kuchukua Sura hizo Kwahyo Kuna Pnemonia Ambayo ni suddenly onset "Acute severe Pneumonia" na hii ndo Pneumonia Hatari kuliko zote kwa sababu inatakiwa Kuwahi matibabu kuliko kawaida..

Huenda mwanao alipaliwa Na maziwa Mara kadhaa na kupata Aspirational Pneumonia ambayo ilisababisha Iwe acute onset..

Kuna Research kadhaa zimefanyika Kwa baadhi ya watoto (Infants)Hufariki kwa Sababu ya Milk Aspiration ambayo hupelekea Aspiration Pneumonia na mara nyingi hawa watoto hupata Acute Lung Failure..

Kuna mambo mengi ya Kuelezea Lakini jibu la Moja kwa moja ni kwamba Inawwzekana kabisa kutokea hivyo..

Kama utakuwa una swali unaweza kuuliza
 
shukrani kwa maelezo ya kitaalamu
 
Pole sana kiongozi kwa msiba! Pneumonia ni bacterial au viral infection na haiji ghafla tena inaambatana na homa na kukohoa sana. Kwa maelezo yako kwa haraka inaweza kuwa ni Aspiration ya maziwa ya kichanga, yani amenyonya na maziwa yakaenda kwenye njia ya hewa badala ya tumboni. Hii mara nyingi inawapata wamama wanaozaa mara ya kwanza endapo hawajafundishwa namna ya kunyonyesha sawasawa. Inatokea kwenye positioning ya namna mtoto anavyowekwa wakati ananyonya au pia ananyonya wkt analia so maziwa yanakosea njia matokeo ya aspiration ni kifo na au huduma za haraka sana za ICU. So kwa namna yyt vituo ulivyotaja havina competence ya kufanya hizo huduma kwa vifaa, tech na staffing unless kungekua na nurse aliyespecialize kuhudumia watoto, wana uwezo wa kusaidia hata kwenye mazingira magumu ya upungufu wa vifaa ambao pia ni wachache sn kwa nchi yetu.

Maelezo mazuri, na ni moja ya kitu cha kwanza kufikirika.

Ingawa umri wa mtoto ni muhimu pia kwenye hili(ni rahisi sana kwa mtoto chini ya mwaka mmoja).

Kuna mambo mengi huchangia pia ya kuongeza:
1: Mama kunyonyesha akiwa amelala kitandani. Mtoto hushindwa ku-control mpangilio wa mwenendo wa maziwa na hatimae kwenda kwenye njia ya hewa.

2: Mama kunyonyesha na kupitiwa na usingizi. Kumwachia ziwa na kumwelemea mtoto na hivyo kushindwa ku-control maziwa pia.

3: Mama kunyonyesha na kumlaza mtoto mara tu baada ya kunyonyesha bila kumbeulisha hewa ndani ya mfumo wa chakula. Mtoto anapocheua maziwa na hewa huenda kwenye njia ya hewa.

4: Mama mwenye maziwa mengi kutokuwa makini ku-control kiasi cha unyonyaji wa mtoto na hatimaye kwenda kwenye njia ya hewa.

5: Hii huwapata pia watoto wenye changamoto wa mfumo wa kimaumbile kwenye njia ya chakula, hewa na moyo wakati wa kunyonya.

Hii hutokana na mfumo wa chakula na hewa kuwa havijawa na uimara wa kutosha kudhibiti kazi yake mahsusi pia mtoto kutokuwa na uwezo mkubwa wa kujitetea kama kujigeuza.
 
Alikuw nazo mda wote na usiku hakuwa na barid bal kutokana na joto kali lililokuwepo mwez uliopita alikuwa anatoka jasho sana usiku
Pole sana mkuu,kwa wazazi ni muhimu kuzingatia kumbadilishia mtoto mara kwa mara nguo
hasa kipindi hicho cha joto,sababu mtoto anapotoka jasho linalowesha nguo ya ndani
aliyovaa,hiyo nguo isipobadilishwa inageuka kuwa kitu cha baridi kwenye kifua,kumbuka mapafu ya mtoto mdogo hayajakomaa na hivyo kumletea madhara
sawa sawa na mtoto aliyewekwa sehemu ya baridi.
 
Back
Top Bottom