MchukiaUonevu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 207
- 79
Tumewazoea.Mmmezoea sana kulalamika mnaonewa mnaonewa mmekuwa kama watoto wadogo hata watoto wadogo hawako hivyo.Ndio maana waarabu hadi leo wameshindwa kuwa na umoja na matokeo yake nchi za magharibi zinawaburuza wanavyotaka.Mlianza na na Raisi wa Iraq mkaja kwa Gadafi matokeo au faida yake iko wapi.Hakuna mtu asiyefanya makosa hapa duniani na kufanya kosa si kosa ila linakuwa kosa ukirudia tena hilo kosa.Ndugu wadau,
Ripoti ya tume iliyochunguza tuhuma dhidi ya upotoshaji wa matokeo ya mtihani wa somo la Islamic knowledge kidato cha sita mwaka 2012 inasikitisha. Tarrifa zilizotolewa na Naibu Waziri wa Elimu Ndg.Phillipo Mulugo kuwa tume ilijiridhisha kuwa kulikuwa na hitilafu kwenye mfumo wa computer inazua maswali mengi kuliko majibu. Matokeo ya uchunguzi huu yametoa taswira halisi ya Necta. Katika hali ya kawaida,makosa hufanywa na kila binadamu,lakini pia degree,frequency na mazingira ya kosa ni kitu kingine. Ni jambo ambalo haliingii akilini makosa yafanyike halafu chombo husika kikae kimya hadi watu waandamane ndio haki itolewe. Waislam wamelalamika miaka mingi sana juu ya baraza la mitihani kumezwa na mfumo unaowanyima haki wanafunzi wa kiislam na hata shule za kiislam. Lakini hawajawahi kupewa majibu zaidi ya kukejeliwa,kudharauliwa,na kuitwa majina mabaya. Leo serikali inakuja na majibu mepesi kuwa ni hitilafu ya computer,sijui formula iliyotumika kukokotoa nk. Haya sio majibu ya kutolewa na Waziri,kila mtu anafahamu computer hufanya kazi kutokana na instructions za binadamu. Huwezi kuingiza wrong formula halafu utegemee majibu sahihi,garbage in garbage out!. Tena cha kushangaza system imechagua somo la dini moja tu la "Islamic knowledge",somo lenye vigezo sawa na somo wanalofanya wanafunzi wa dini nyingine la "Divinity".
Hatuwezi kuridhika na majibu mepesi kiasi hiki kwa makosa ya kudhamiria kiasi hiki. Sensitive issues kama matokeo ya mitihani sio kitu cha kufanyia masihara. Hii kazi haifanywi na mtu mmoja,ni jopo la watu,tena wanaofanya kazi independently,na mwisho lazima matokeo yawe reviewed na watu makini. Iweje leo Waziri aseme ni kosa la Mkurugenzi mmoja. Hatuwezi kuridhika kwa kumfukuza kazi mtu mmoja,tunataka uozo uliopo Necta uondolewe,haki itendeke na tena haki ionekane kutendeka!
Tujiulize maswali haya.1:Utaratibu wa Necta ukoje kabla ya kuchapisha matokeo ya mtihani.
2:Ikiwa hii si mara ya kwanza kwa Waislam kulalamika juu ya mfumo kandamizi uliopo Necta,ni hatua gani zilishachukuliwa ku-address uozo huo.
3:Kwa nini watu walewale waliolalamika miaka mingi juu ya mfumo kandamizi wamekuwa proved victims wa mfumo tajwa.
4:Kama wamekiri somo moja tu kuathirika na "hitilafu kwenye mfumo wa computer",tena somo ambalo hufanywa na wanafunzi wa dini moja tu,is there any validity of the results for the rest of the subjects?
Kwa majibu ya Ndg.Mulugo,matokeo ya kidato cha sita yanakosa uhalali wa kuitwa matokeo,na hasa kwa wanafunzi wa Kiislam(huu ni mtazamo wangu).Kuchapisha upya matokeo ya somo moja la Islamic Knowledge hakuniondolei hofu juu ya madhila wanayofanyiwa Waislam na shule za kiislam na baraza la mitihani. Hatuwezi kuamini kirahisi kuwa makosa yalifanyika kwenye somo moja tu,na hasa ikizingatiwa nature ya kosa lenyewe limekuwa "too selective".Tunatakiwa tujiridhishe beyond reasonable doubt kuhusu muundo wa Necta,ufanyaji kazi wake,watumishi wake,usahishaji mitihani,na uchapishaji wa matokeo ya mitihani.
Nawasilisha!
Hivi mpaka muambiwe kwa namna gani ndiyo muelewe? Mmeambiwa kwamba, awali somo la Islamic Knowledge lilikuwa na mitihani mitatu, hivyo program ya kukokotoa wastan ilikuwakuwa inagawanya kwa tatu...Lakini kuanzia mwaka jana, somo hilo lina mitihani miwili tu...sasa kilichotokea ni kosa la kitaalam yaani: hawakubadilisha ile program ya kukokotoa wastani wa mitihani mitatu kitu kilichopelekea hata huu mtihani huu wa islamic knowledge ambao una mitihani miwili kukokotolewa wastani wake kama vile kuna mitihani mitatu. Kwanini mnahangaika na kitu kilichotolewa maelezo ya kujitosheleza mara elfu?
Hili linaeleweka. Ukitizama kwa makini tatizo hili unaona kuwa hakuna "effective controls". Kukosekana huko kwa effective controls kunafanya mtu ajiulize, je kuna makosa mangapi ya namna hiyo yanatokea au yatatokea tena? Maana masomo na hata namba ya hizo papers potentially ni vitu vinavyobadilika achilia mbali mifumo yenyewe ya computer! Vipi kuhusu usahihishaji......controls zipo effective kwa kiasi gani? Zinaweza kuzuia makosa (ya 'kibinaadamu'!) kwa kiasi gani?Hivi mpaka muambiwe kwa namna gani ndiyo muelewe? Mmeambiwa kwamba, awali somo la Islamic Knowledge lilikuwa na mitihani mitatu, hivyo program ya kukokotoa wastan ilikuwakuwa inagawanya kwa tatu...Lakini kuanzia mwaka jana, somo hilo lina mitihani miwili tu...sasa kilichotokea ni kosa la kitaalam yaani: hawakubadilisha ile program ya kukokotoa wastani wa mitihani mitatu kitu kilichopelekea hata huu mtihani huu wa islamic knowledge ambao una mitihani miwili kukokotolewa wastani wake kama vile kuna mitihani mitatu. Kwanini mnahangaika na kitu kilichotolewa maelezo ya kujitosheleza mara elfu?
Hivi mpaka muambiwe kwa namna gani ndiyo muelewe? Mmeambiwa kwamba, awali somo la Islamic Knowledge lilikuwa na mitihani mitatu, hivyo program ya kukokotoa wastan ilikuwakuwa inagawanya kwa tatu...Lakini kuanzia mwaka jana, somo hilo lina mitihani miwili tu...sasa kilichotokea ni kosa la kitaalam yaani: hawakubadilisha ile program ya kukokotoa wastani wa mitihani mitatu kitu kilichopelekea hata huu mtihani huu wa islamic knowledge ambao una mitihani miwili kukokotolewa wastani wake kama vile kuna mitihani mitatu. Kwanini mnahangaika na kitu kilichotolewa maelezo ya kujitosheleza mara elfu?
Hebu tuwe objective kidogo wajameni. Hivi haya malalamiko yote ambayo yanatolewa na hawa ndugu zetu, ni kwamba hayana mantiki? Mtu anaamua tu kulalama out of the blu? Ilitokea kidato cha 4, sasa cha 6 kwa somo hili moja. Hamuoni kuwa kuna tatizo. Is it possible kwamba average ya masomo mawili igawanywe mara tatu, na mhusika asigundue hilo. Vipi pale wanapofanya review kabla ya kutangaza rasmi matokeo? Hawafanyi tathmini na kubaini kwanini wanafunzi wamefaulu sana au kufeli sana somo fulani. Mtu akilia kuwa anaonewa, hebu msikilize kwanza kama hoja za msingi zipo. Kama hazipo, potelea pote. Ila ni dhahiri kuwa kuna tatizo linalowahusu Waislamu na jamii (dunia) inafumba macho na kuziba masikio. For what reasons, God knows.
Hivi mpaka muambiwe kwa namna gani ndiyo muelewe? Mmeambiwa kwamba, awali somo la Islamic Knowledge lilikuwa na mitihani mitatu, hivyo program ya kukokotoa wastan ilikuwakuwa inagawanya kwa tatu...Lakini kuanzia mwaka jana, somo hilo lina mitihani miwili tu...sasa kilichotokea ni kosa la kitaalam yaani: hawakubadilisha ile program ya kukokotoa wastani wa mitihani mitatu kitu kilichopelekea hata huu mtihani huu wa islamic knowledge ambao una mitihani miwili kukokotolewa wastani wake kama vile kuna mitihani mitatu. Kwanini mnahangaika na kitu kilichotolewa maelezo ya kujitosheleza mara elfu?
Muhusika mkuu kwenye hicho kitengo cha ukokotoaji ameshawajibishwa...unataka nani mwingine aondoke/asimamishwe kazi? Shukuru Kawambwa , Mlugo au Ndalichako???Huo wote uliouongea "collectively" unaitwa neno la kiswahili "U Z E M B E " na mtu akiwa mzembe lazima awajibike! na si kitu cha ajabu! wamewajibika wengi hasa upande wa wenzetu kule visiwani kwa kuwa wale waungwana, huku kwetu bara mtu mpaka AWAJIBISHWE!
Basi fanyeni mnachotaka. Mnatukera mnavyotuletea hapa malalamiko yenu. Mkishauriwa mnakuwa wabishi...fanyeni mnachotaka...yameshatokea!
Muhusika mkuu kwenye hicho kitengo cha ukokotoaji ameshawajibwa...unataka nani mwingine aondoke? Shukuru Kawambwa , Mlugo au Ndalichako???
Hakuna kitu kama hicho. KIKULACHO KIMO NGUONI MWAKO...Tafakari