Ndoa

Baba Kapompo

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
1,344
Reaction score
468
Suala la kuwa na mpenzi waweza amua muda wowote ule utakao lakini suala la ni nani atakaa na wewe daima ni suala la wawili kushirikishana na kukubaliana. Kama mlikutana bar, club au sehemu yoyote ile ya starehe na huyo mpenzi wako kamwe usiamini kuwa ukiingia kwenye mahusiano na hasa mahusiano ya ndoa utaweza kumbadilisha kwa dakika ishirini kama ilivyo rahsi kukubaliana kuingia hotelini na kulala ndani ya dakika hata kumi.

Sumaku hunasa vitu vyenye asili ya chuma na mara nyingi watu twakutana na wapenzi wanaotokana na jinsi sisi tulivyo ingawa wengi hujitahidi kuzificha tabia zetu kutokana na muda mfupi tuutumiao kufahamiana na kisha kutangaza kuwa twataka kuishi pamoja.

Unaweza ukavumilia kwa usiku mmoja na kulala na mtu mwenye kunuka harufu ya pombe, sigara au hata mapungufu mengi aliyonayo lakini huwachukua watu wachache sana kuvumilia hali hizo milele.

Naongea hivi kwani leo kuna mtu akaniuliza inachukua muda gani kwa mtu kuomba talaka na kupewa.... Nilishtuka sana kwani tumemchangia fedha ya harusi mwaka mmoja na nusu uliopita na mbaya zaidi alikuwa na moto wa mapenzi wenye mtetemo zaidi ya simu ya kichina.

Iweje leo aongelee sula la talaka. Guys, suala nyeti na bovu kuhusu maisha yetu ya mahusiano ni kwamba twatumia mizani feki kwa vitu vyenye kuhatarisha mahusiano yetu na hata furaha na uhuru wa maisha yetu ya baadae.

Wengi twatamani sana ndoa sio kwa maana ya kuelewa maisha ya ndoa ila kuchangiwa zawadi ukumbini na kuona umewaziba midomo watu na kuwa sasa una mke au mme. Idadi kubwa ya kina dada wao huamini anapoingia katika mahusiano huenda kumbadilisha tabaia mwanaume na baada ya kujaribu na kuona ameshindwa kumbadilisha awe kama vile atakavyo huna na ndoa imeisha.

Na haya ni matokeo ya mahusiani ya siku mbili kwenye safari ya gari moshi yanayozaa ndoa bila hata ya watu kufahamiana. Kwa mtazamo wangu nafikiri kabla ya kufikia maamuzi ya kuoa au kuolewa ni vyema kupata muda wa kufahamiana na huyo mwenza wako kwa muda na kujuana vilivyo hasa tabia, maono, historia zenu, itikadi, elimu zenu, uwezo wenu wa kutambua mambo na jinsi ya kukabiliana nayo.

Inanishangaza ukaingia bar meza tatu tofauti wote wanajadili jinsi mahusiano yao yalivyomabovu na wengine wakidiriki hataka kutoa siri za wapenzi wao .... inatisha sana na kuwakatisha tamaa wale ambao hawajaoana au hata wale wanaofikiria kuoana na kuona ndoa ni jeshi dogo.

Mwisho suala la ndoa ni jinsi wewe unavyotaka iwe ukimshirikisha mwenzio... mnaweza kuchagua furaha, kuheshimiana na kutatua matatzo yenu wenyewe na hutaliweza hili kama huna mapenzi ya dhati kwa mwezio.

Hebu tuukatae ule usemi wa sasa kuwa ndoa nyingi za sasa zasababishwa na mimba wapendano wajitambue na kusema ndoa yao ilitokana na wakati, kupendana na baada kufanya tathmini ya kuwa sasa wanahitaji kuwa pamoja.
 
maelezo marefu ajifunze kuandika kwa kifupi inachosha ingawa kuna ujumbe ndani yake
Acha tu somo la kuendesha gari hili, unapodrive unakanyaga mafuta sawa eeh ila kabla ya kurudi rivasi hakikisha umewasha gari kwanza, tuko pamoja mpaka hapo?
 
Ndo kwanza kunakucha. Ni leo ya saa ngapi?
 
Hivi mama yangu na baba yangu wameshindwa kunibadilisha halafu uje kunibadilisha wewe tuliyekutana tukiwa tushaota meno 32!

Tuache masikhara
 
Hivi mama yangu na baba yangu wameshindwa kunibadilisha halafu uje kunibadilisha wewe tuliyekutana tukiwa tushaota meno 32!

Tuache masikhara

Naweza kukubadilisha. Na wanasema wapendanao n.kama mapacha that means tabia ziko sawa na kila kitu usifikir utaweza kukaa na mtu ambae ww unafikiri kulia yy kushoto hamdumu na namaanisha kua ukimpata unaendana nae utabadilika tu
 
Kuna tabia nyingine zinaweza kubadilika na nyingine huwezi kabisa kumbadilisha mtu. Naukisha kubali kuingia kwenye ndoa pia ukubali madhaifu ya mwenzako. kumbadilisha mtu ni mungu mwenyewe.
 


Hebu tuukatae ule usemi wa sasa kuwa ndoa nyingi za sasa zasababishwa na mimba wapendano wajitambue na kusema ndoa yao ilitokana na wakati, kupendana na baada kufanya tathmini ya kuwa sasa wanahitaji kuwa pamoja.


Laiti wana ndoa wengi wangeyajua haya kusingekua na. Mitafaruku ya ajabu ajabu
 
baadhi hufikiri ndoa ni kujimilikisha kugegedana.......hawajuani ila wanakariri watu waliooa bila kujihakikishia ni nini hasa maana ya ndoa.....ndoa ni zaidi ya kuzimu ya duniani....sio papara, watakuchangia kila kitu ila maisha ni yako......suala la kunibadilisha ni gumu........ nenda tuu.... tabia zangu niachi......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…