Tafiti nyingi zinaonesha kwamba wanaume wengi huingia kwenye ndoa bila ya kutarajia, wakati wanawake ni moja ya mipango yao ya maisha tangu wakiwa washichana wadogo. Kwenye ndoa wanawake wanakuwa na mipango tofauti sana na wanaume. Ukija stuka wote hawaitamani ndoa nyumba inakuwa kama jela vile.
Ni nani hasa kati ya mwanamke na mwanaume ambaye anasababisha hadi ndoa ionekane ni taasisi yenye dhahama nyingi kuliko raha?