Ndalichako hawafahamu "MASKINI:

HUU ni ukiukwaji wa taratibu za elimu na filopsofia zake.Maamuzi kama haya yakitekelezwa yatadumaza uwezo wa kufikiri na kung'amua maarifa na ujuzi.Mtu hashindwi kujifunza maarifa mapya labda awe amevia akili.Si vizuri kuweka vigezo vya lazima wakati mtu hujifunza maarifa kwa utashi na haiba yake kwa kupendelea soko la ajira.Elimu ni mnyumbuliko na haina mwisho.Ndiyo maana inatungiwa sera zake.Kama sera ni mbaya hazifuatwi kwa kuwa zinadumaza maendeleo ya watu kielimu na Taifa kwa ujumla.
 
akili mbovu lect wangu alekua ananifundsha practical ya chemistr kaanzia ngazi ya cheti.
. lakini atakuja Lizaboni atasema ndalichako yuko sahihi
 
Aisee umeongea maneno ya busara sana. Lakini nmeangali clip, ni fupi lakini nadiriki kusema Mh HAKUSEMA hayo tuliyafikiria na kuyajadili. Hata hivyo, mjadala huu umesaidia kwa kiwango kikubwa viongoz wetu wajue Watanzania wanafuatilia ustawi wa nvhi yao. Kauli yoyote tatanishi itazua mjadala tu.
 
Yamewafika pabaya sasa mnamtafuta mama wetu ubaya, mama anafanya kweli na ni lazima elimu iheshimiwe na watu wote.
 
Mi naona mama yuko sawa haiwezekani mtu ana D NNE yaani div 4 mbovu.....aunge unge cert aje Diploma halafu apate degree,,huku kidato cha NNE alipata alama mbovuuu.....
Man una talk as if diploma is for free... nenda vyuo vya ufundi man.. diploma kuipata ni ume hustle. Alaf si wote wanaosoma diploma wamefeli... wengine walifaulu form 4 tena div 2 lakin hawakutaka kwenda advanced..
 
Mi nachojua diploma ngumu ni ya ualimu tu...hizo zingine mnapewaga tu.....

Bhasi tuache kuchukua 4 mbovu kujiunga na Certificate
Umekariri brother.... embu nenda dit... kacheki diploma zao zilivyo... alaf ndio urudi hapa
 
Reactions: Ame
Acheni unafiki nyie sindiyo mlikuwa mnakesha JF kumuomba rais Magufuli amchague kuwa waziri.

Sisi tunamjua siku nyingi tuliwambia kuwa huyu dada ana matatizo mlitushambulia sana.

Tulieni sasa mnalia lia nini.
Ha ha ha ha [emoji40] [emoji40] [emoji40]
 
Unataka kuniambia huko diploma huwa hawafanyi mitihani ya kuchujwa na wasiofaa kutupwa nje??

Hebu kama una mtoto anaesoma au aliyekwisha kusoma chuo muulize kuhusu hao watu waliotokea diploma huwa wanakuwa vipi darasani?
Miaka niliyosoma mimi walikuwa wanaondolewa karibu wote 1st year kwaku disco . . . . Yaani akikatiza physical chemistry , statistics na engineering ujue lazima alipitaga A level otherwise utaona tu rangi nyekundu . Sijui siku hizi
 
Mi naona mama yuko sawa haiwezekani mtu ana D NNE yaani div 4 mbovu.....aunge unge cert aje Diploma halafu apate degree,,huku kidato cha NNE alipata alama mbovuuu.....
Kwa taarifa yako MTU anaweza toka darasa LA saba hadi pale mwisho unapopajua wewe kielimu na akawa bright,tens hao waliowengi wanakuaga vichwa mpaka unashangaa,alafu mabadiliko ya elimu hayafanywi haraka HVO ni mfumo ubaobadika kidogo kidogo kwa awamu,huwezi amka tu asubuhi ukaja na mabaduliko yako,unahitaji kuwajuza watu mbalimbali wadau katika elimu,mabadiko kila kukicha wakati huo huo mazingira wezeshi ni yaleyale,hakuna maabara,vitabu,walimu wachache na walioko bado sana malalamiko yao,mfano kubasilisha tu GPA ilitakiwa ichukue hata miaka miwili na kuwafanya wale waliokuwa wanasoma kipindi cha GPA kabla haijabadilishwa wamalize kabisa then wanaojiunga nyuma yao ndio wakumbane na hayo mabadiliko,sasa huyu mama toka ameingia mabadiliko yaliyotokea hata kumi yanafika just kwa mwaka mmoja tuu,hata madogo wanafaulu hata chuo hawaingii,waliomaliza darasa ma saba wengi wamekosa nafasi,sasa sijui lengo lake ni nini? Mara mia hata Mungai au murugo sio huyu mama
 
Hata ukiwa kazini na una cheti au diploma unaweza kusoma five &six hatimae ukapata vigezo vya kusoma digrii. Watanzania wenzangu tupunguze kulalamika kwa kila kitu, nani alikwambia maskini hawezi kifaulu? Wasomi asilimia kubwa vyuoni wamesoma shule za kata.
 
Ama kweli watu wanapenda sana kulinda maslahi yao binafsi badala ya kuangalia maslahi mapana ya Taifa. Ukweli ni kuwa alichosema Ndalichako ni cha msingi kwa mustakabali wa elimu ya Tanzania. Tatizo wako watu wengi sana wenye elimu ya kuunga unga sasa wanaona Profesa Ndalichako anaweka wazi siri zao. Hilo ndilo tatizo la watanzania walio wengi ubinafsi umewatawala. Wote wanaopiga kelele wachunguzwe kama hawana elimu ya kuunga unga. Vyeti vingi lakini havina ufanisi wowote ndiyo maaana taifa letu liko hapa lilipo sasa. Linasema linawasomi lakini hawana tija kwa taifa letu. Kisa ni kuwa wana vyeti lakini hawajaelimika. Mpango wa Ndalichako ni wa kulikomboa taifa na kuondoa watu wasio na sifa kuendelea kuliharibu taifa. Ni hao hao ndio waliweka graduation kuanzia kindergaten bila hata kujua gratuation maana yake ni nini. Prof. Ndalichako Nakupa Big up. Songa mbele. Umetupa jiwe kwenye kundi la watu wenye vyeti bila kuelimika sasa wanapiga kelele kwa kuwa jiwe limewapiga mahali pachungu.
 
wenye elimu ya kuunga unga siyo maskini acha kusingizia maskini.
 

Huo ndio ukweli. Watanzannia hawapendi kuambiwa ukweli haswa pale maslahi yao yanapoguswa. Mfumo wa elimu ya Tanzania ulikuwa mbovu kabisa. Sasa Prof. Ndalichako anaturudisha kwenye mstari tunalalamika. Mimi binafsi sitaki mwanangu asome katika mfumo huu wa kuunga unga. Watu wafuate utaratibu. Pili chuo kikuu siyo cha kwenda kila mtu. Elimu ni aina fulani ya ubaguzi unaokubalika. chuo kikuu watu hawaendi kwa miguu wanakwenda kwa vichwa. Ukweli huo ubaki kuwa hivyo. Ni mara ngapi tumeona watu wanamaliza chuo kikuu lakini hawana uwezo wa mtu wa chuo kikuu? wakienda kwenye profesional studies wanafeli kabisa unajiuliza walipitaje chuo kikuu hupati majibu. Watu wasome huo ndio ukweli.
 
huyu mama, kabla hajawa professor alikuwa naakili zake vzr, na alijijengea heshima kwnye jamii, sasa huu uprofessor unampa shida, miakili imemwagika...
 

Afadhali umeliona hili, halafu wanao support hili bila tafakari pana wajue tu kuwa kuna watu/wanafunzi katika hao wanaoonekana kuwa ni failures ambao darasani walikuwa na uwezo kuliko hata waliopasi, aidha walipatwa na shida kipindi cha mitihani, au kufelishwa lakini sio wajinga kama wanavyotaka kuamini wengine. Na vile vile pia ijulikane kuwa zimekuwako pia hizo div 1,11 za kununua mitihani au matokeo, labda tujifanye kuwa hatujui hilo.
Na hata hivyo hizo certificate na Diploma kwani ni za bwerere kiasi hicho? Mbona nyingine zinahitaji kamsuli flani mwanafunzi aweze kupasi, mi sijazipitia hizo ila nawaonaga wanavyojipinda waweze kufaulu. Kuna maswala mengi sana ya kuchangia kwenye elimu kama ni mjadala, hata kuna tetesi pia kuhusu uzembe, hongo, uonevu necta kwenye usahishaji, ni maneno na shuhuda za mitaani lakini source ni hao hao wasahishaji. Kuna kipindi mi binafssi nilimsikia mwl mmoja akisema kuwa hawaweki umakini kwenye usahishaji kisa wanapunjwa malipo, sasa hapo wanafunzi hasa wa kayumba unategemea wapate haki kwenye usahishaji hapo? msimamizi anaingiza mafurushi aki alert wasahishaji hii ni shule flan jaman attension?! Any way kuna mengi
 
Zama zake hizi mwacheni afanye anachotaka akimaliza mihula yake ya kiutawala tutarudi kwenye zama zetu za kuungaunga .

Hayo matamko yao wala sio msahafu kusema will never be amended.
 
Mi naona mama yuko sawa haiwezekani mtu ana D NNE yaani div 4 mbovu.....aunge unge cert aje Diploma halafu apate degree,,huku kidato cha NNE alipata alama mbovuuu.....
wewe una unafiq mpaka basi, wewe unajua mazingira ya kupata form four dddd? kuna watu wakiletwa dar wakapata tuishen wanapasua, mtu anatoka vijijini alikuwa na akili lakini wakampeleka shule za kata walimu hakuna unategemea nini?
 
Huyu mama ndiyo anaharibu kabisa kupita kiasa, huyu sidhani kama anashaurika hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…