Nchi ya Vilio

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,902
Reaction score
40,555
Rais alipokuwa Tandahimba - ALISIKIA KILIO CHAO.
Rais alipotembelea Masasi - ALISIKIA KILIO CHAO.
Rais alipokuwa Mtwara mjini - ALISIKIA KILIO CHAO.
Rais katoka Mtwara kaingia Lindi - AKASIKIA KILIO CHAO.
Rais kafika Mtama - AKASIKIA KILIO CHAO.
Rais kaenda Mafia na Rifiji - AKASIKIA KILIO CHAO.

Kwa Muda wa siku 6 alizokaa Mtwara na Lindi ni vilio, vilio, vilio na vilio.

Hata wale kina mama waliofanya igizo la kumpenda Rais kupita kiasi WALILIA KILIO.

Kule Kwa Waziri mkubwa ambako ameambiwa huko changamoto zolishaisha, lakini nako ALISIKIA KILIO CHAO hadi akaahidi kumuenzi Mtu ambaye bado yuko ofisini.

Ni Kwa nini viongozi wa nchi hii wanajivunia na kuona fahari ya kuongoza watu Wenye VILIO? Vilio vina faida gani Kwa watawala Hadi wapende kuvisikia Kila wanakokwenda? Naamini Rais atakaporidi Mtwara na Lindi baada ya miaka 2 ATASIKIA KILIO CHAO.

Ni lini na wapi atasikia VICHEKO? Kwa nini Watanzania hawana VICHEKO? Au hivi VILIO anavyosikiw Rais ni VILIO VYA FURAHA? Maana nasikia kuna watu wakifirahi Sana huwa WANALIA!

Lakini Kwa hili la Watanzania sidhani. Maana kama kingekuwa KILIO CHA FURAHA Rais angesema nimeona FURAHA yenu.

Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba Watanzania HAWANA FURAHA, WANA HUZUNI, WANA VILIO Kila mahali. Si Mtwara na Lindi pekee, Watanzania Wana VILIO;

Mwanza
Kigoma
Dodoma
Manyara
Singida
Morogoro,
Dar
na
LOLIONDO.
 
Chama cha maigizo(CCM)
 
Inawezekana vilio vyao ni vya kutaka kila mara aonekane huko angalau wapewe tena kanga na teni teni kwa siku kadhaa milo miwili yaweza patikana.nje ya hapo ni ngumi jiwe tuu hadi uchaguzi ukaribie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…