Nawezaje kuwasilisha wazo langu la tangazo kwa kampuni za mawasiliano?

Mzee wa old school

JF-Expert Member
May 16, 2021
508
834
Wakuu habari zenu! Mimi nina script ya tangazo la mitandao ya simu. Sasa nafanyaje nipate kuwasilisha hilo jambo?

Kwa anayefahamu tafadhali.
 
Kabla ya yooote hakikisha unaenda Copyright Society of Tanzania (COSOTA) kwa ajili ya kisajili hiyo script yako kisha baada ya usajili ndio uende sasa huko mtandao wa simu.
Ukifika huko hakikisha unatumia proper channel kufikisha hiyo kazi yako kwa wahusika sio mnapeana kichochoroni, hakikisha kabla ya kukabidhi hiyo kazi unakua na 'non disclosure agreement' na hii iambatane na dispatch wakati unawasilisha. Baada ya hapo kaa utulie kama itapita basi fanya nao kazi na ikikataliwa pita hivi.

Kila la kheri
 
Hizo ofisi za COSOTA zipo pale Kivukoni katika jengo la Utumishi mahali kulipokua ofisi za sekretarieti ya ajira. Fika hapo watakupa maelezo ya namna ya usajili, namba yao ya ofisi ni 0738015014
 
Shukrani mkuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…