Whatsapp imekua ni moja kati ya teknolojia inayotuunganisha marafiki. Wengi wetu tumenufaika na huduma zake mbalimbali ikiwamo GROUP CHAT.
Hapo nyuma kidogo niliwahi kuanzisha group la marafiki ambalo kwa kweli limetujenga na kutuburudisha. Nimeweka uzi huu jamvini kupata msaada wa namna gani nitampa member mwingine (nimtakaye) ukuu wa group lile. Kwa mujibu wa Whatsapp mkuu mpya hupatikana randomly baada ya yule wa zamani kujitoa. Hivyo kama menye mbinu za medani kufanikisha nilitakalo atusaidie.