Wadau,bahati mbaya au nzuri sikufanikiwa kukiuza kile kiwanja alijitokeza mdau mmoja tu na akasema hajalipenda,however kuna kitu kilijitokeza miezi miwili tokea nitangaze hapa watu walijenga kwa kasi sana wakuu mitaa ile lkn pia alijitokeza jamaa mmoja akatoa ofa ya milioni 30,lakini nikawa ile biashara niliyotaka kufanya na ile hela ikawa imeshapotea so nikaghairi na nimeamua kujenga mwenyewe....ila ki ukweli wadau viwanja maeneo ya Goba kinzudi vipo,lakini vinapanda bei kwa kais sana,
kwa mfano,kiwanja changu nilinunua mwaka jana august,kwa bei ya milioni 10,lakini mwaka huu mwezi wa kumi nimepata ofa ya milioni thelathini,hii inaweza kuwa biashara nzuri!
Pia nina kiwanja kingine maeneo hayo nilinunua kwa bei ya milioni mbili na nusu kwa mtu huyo huyo,hichi nacho kiko kama kilometa tatu kutoka hapo goba kinzudi,now nimepata ofa ya milioni tano na nusu...
sasa ukiangalia kwa makini utagundua kuwa viwanja vinapanda sana,na ukitaka kununua kiwanaja usiangalie sana watu wanafanya nn,maana unaweza kukatishwa tamaa...nitoe tu ushauri kama una nafasi weekend,nitakupatia namba ya mtu kule kinzudi ni kijana wangu wa site then uwasiliane nae atakuzungusha uone viwanja mbali mbali.
just PM me