Mkuu hakuna gari inaitwa Harrier Lexus. Kuna matoleo yanayofanana kama Toyota Harrier na kuna Lexus RX. Hizi ni gari mbili tofauti, moja inatengenezwa na Toyota, na nyingine inatengenezwa na Lexus ambayo pia ni kampuno ya Toyota. Baadhi ya spear zinaingiliana, lakini kuna spear kama radiator na nyinginezo haziingiliani. Lexus RX ni luxury zaidi ya Toyota Harrier.
Ni sawa na Mercedes Benz kuna matoleo au models zao wanatengeneza pia AMG na sio Mercedes zote ni AMG.
Hiyo gari yako ni Toyota Harrier, na namna nzuri ya kuitambua ni kutumia hicho kioo kwenye boneti. Lexus RX huwa hazina kioo kwenye boneti.