Mgagaa na Upwa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 16,331
- 35,865
Mkuu nimekuelewa kwenye huo mfano wako wa Azam fc, ila kuna haya maswali hapa unaonaje ukatusaidia kuyajibu kwa maana ni kama unajua nini kinachoendelea huko ila pengine sisi wengine hatujui. Hebu ingia uzi huu hapa ukatujibie maswali yetu au yeyote anayejua atusaidie.Yanga inabadilishiwa mfumo wa umiliki na uendeshwaji tu sio kuuzwa au kukodishwa . Mfumo uliopo ni wanachama kupitia uongozi waliouchagua kuimiliki na kuiendesha klabu kwa asilimia 100.
Sasa inakwenda kumilikiwa na mtu mmoja kwa asilimia 75 na 25 zikibaki kwa wanachama .
Mkataba husika kuendeshwa kwa miaka 10 ni sawa na ubinafsishwaji wa sehemu ya umiliki ili klabu ijiendeshe kwa faida kama yalivyofanyiwa mashirika ya Umma mwanzoni mwa miaka ya 90.
Kilichopo ni kuhakikisha " Brand " ya klabu inakua kwa haraka na faida kwa mwekezaji husika na klabu.
Miaka 81 hakuna la maana hata Azam FC yenye miaka 8 chini ya mtu mmoja inajeuri ya kuongea sasa tuache hii miaka 10 tuone nini kitafanyika .
Watu wanasema atapata faida kubwa sana na sisi kuendelea kubaki masikini . Kwa miaka 10 ametoa pesa sh ngapi ambazo hazijampa faida yoyote zaidi ya umaarufu?!
Tulipofikia hata kumuuzia ingewezekana poa tu maana walibaki wachache wananufaika timu inazidi kuwa masikini bila maendeleo yoyote.
View attachment 377116
Umesema kweli mkuu... Lakini acha tumpe timu tu, hakuna namnaKatika kikao walichokaa cha Kuikodisha Timu ya Yanga kwa Mkodishaji kati ya wateja wanaotaka kukodishwa Yanga na Wenye timu ya Yang a , Mtu mmoja aitwae Manji alihudhuria kikao hicho kama Mkodishwaji Mkuu (Tenant) na pia mtu huyohuyo alihudhuria hicho kikao kama Mkodishaji Mkuu(Landlords).
Akiwa kama Mkodshwaji Mkuu (Tenant), Mtu huyo aliweka terms za mkataba anaoutaka (proporsals) yeye mteja ambao alidhani kama Mkodishwaji Mfanyabiashara angefaidika nao, lakini Mtu huyohuyo mmoja akiwa kama Mkodishaji Mkuu (mwenyemali) ambae alitakiwa kufikiri kwa faida ya wenye mali wenzie alikubaliana na terms/proporsal zilizowekwa na mteja ambae nae ndio yeye yeye mwenyewe!!
Yaani katika Meza ya majadiliano iliyohusisha pande mbili za Landlord v/s Tenant, mtu huyo ikifika zamu ya Landrod kuongea basi anahamia upande wa Yanga na anaanza kuongea kama mwenyekiti na anatoa hoja, na ikifika zamu ya tenants kuongea basi nae ananyanyuka kwenye kiti na kuhamia upande waliko wafanyabiashara wenzake anaongea kama tenants Mkuu akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa mwenyekiti ambae ni yeye mwenyewe.
Na wakifikia makubaliano basi katika Mkataba mtu huyohuyo anasaini sehemu ya Landlord na anasini sehemu ya Tenants. Yaani Mwenyemali Mkuu ni yeye, na mteja Mkuu ni yeye pia,