Jinsi ya kuchagua pump kwa ajili ya matumizi yako ya umwagiliaji!
Image source: mtandao.
Kabla ya yote, Kuna huu uzi ambao pia ulikua unaelezea kilimo cha umwagiliajai kwa ujumla
Special thread: Kilimo cha umwagiliaji (Irrigation)
Ni ukweli usiopingika katika kilimo cha umwagiliaji, pump ni kama moyo au sehemu ya muhimu ya umwagiliaji! Pia pump inachukua kiasi kikubwa katika bajeti ya kuanza kilimo cha umwagiliaji, hivyo ni vyema tukachagua pump ambayo hatuwezi kujutia baada ya kuinunua!!! Hizi ni njia ambazo unaweza kuzitumia wakati unachagua pump kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji!
1. Price/gharama.
Ni ukweli usio pingika kwamba kwa sasa kutokana na soko huria, bidhaa moja inaweza kuwa na bei tofauti kulingana na duka! Hapa lazima uchague pump ambayo utatumia gharama ndogo ili kubata ubora unahitajika. Lakini pia ni vyema ukajua unapoangalia bei pia zingatia ubora wa pump!!
2. Fuel/Mafuta
Pump nying zinatumia mafuta ya diesel au petrol! Sasa hapa unatakiwa ujue kati ya petrol na diesel ni wapi patakua rahisi kwako hasa katika swala la gharama! Je petrol ni shilingi ngapi kwa lita? Je diesel ni shilingi ngapikwa lita? Ni ukweli kwamba engine inayotumia diesel ina ufanisi/efficiency mkubwa kuliko injini ya petrol!
Kama hiyo haitoshi kuna pump ambazo zinatumia umeme na nyingine zinazotumia solar/umeme wa jua! Hapa unatakiwa uamue moja ambayo itakua rahisi kwako!
3. Operation/matumizi
Kuna pump unatumia manually na nyingine unaziwasha na kuacha ziendelee kufanya kazi! Kuna pump kama money maker pump ambazo nguvu yako inahitajika ili ifanye kazi, ila nyingine mfano za petrol na diesel haziitaji uzi-operate manually!!
4. Matengenzo/service
Je pump unayotaka kuinunua inatengenezeka kwa urahisi? Pump kama mashine nyingine inafika kipingi zinaharibika kwahiyo ni vyema unaponunua uangalie je inatengenezeka kwa urahisi? Je vifaa/spare vyake vinapatikana kwa urahisi??
5. Ukubwa wa eneo!
Shamba likiwa kubwa maana utahitaji pump kubwa zaidi, na shamba likiwa dogo utahitaji pump yenye uwezo wa wastani!
Kutoka kwenye manual book ya pump aina ya honda…
Sunction port diameter.
Hiki ni kipenyo cha sehemu ya kuvutia maji. Kama tunavyoona imeandikwa 2 inches, hizi zinatofautiana kulingana na ukubwa wa pump, inaweza kuwa Zaidi ya 2inches!
Delivery port diameter.
Delivery port ni sehemu au tundu la kutolea maji kutoka kwenye pump!
Total head.
Huu ni umbali kwenda juu, ambapo pump ina uwezo kusukuma maji, kwa case yetu ni futi 64 sawa mita 50!
Delivery head.
Huu ni umbali (vertical distance) ambapo pump inauwezo kusukuma maji. Umbali huu unaanzia kwenye delivery port.
Sunction head.
Huu ni umbali ambao pump inaweza kuvuta/kuvyonza maji kutoka kwenye chanzo kama mto, bwawa, mfereji n.k. mara nyingi huwaga mfupi kuliko
delivery head!
Discharge capacity!
Hii ni sehemu ya muhimu ya pump. Hapa tunaonyeshwa uwezo kamili wa pump, je pump ina uwezo wa kusukuma maji kiasi gani je ndani ya muda gani?? huwa inaandikwa interms of discharge/flux per time! kwa mfano hapo juu pump yetu imeandikwa
discharge capacity equals to 500 litres per minutes! kwa lugha nyingine tunaweza sema pump yetu ina uwezo wa kutoa lita 500 kwa dakika! hii inatofautiana pump na pump pia inaweza wekwa kwa vipimo tofauti yaani ft/min au Miter cubic per hour n.k.
Priming.
Hikini kitendo cha kuondoa hewa ambayo ina madhara makubwa sana ndani ya pump! Kuna pump lazima utoe hewa manually na nyingine ni automatic!! ni vyema ukachagua pump inayotoa hewa yenyewe (automatic priming)!
Image source: google