Maisha tu Mkuu kama nilivyosemaKapotelea wapi huyo mchumba?!
Mkuu, kwa kawaida huwa tunatafuta ambavyo hatuna na au hatujawahi kuwa navyo.Una mtafuta wa nini wakati ujawai kuwa nae
Ni kweli Mkuu ila naamini inawezekana pia kupata huku online. Shuhuda za watu waliopata wenzi online ziko nyingi tu,jambo la msingi ni kuwa makini.Nakuomba usikate tamaa Mkuu,popote waweza pata mwenzi iwe kanisani,msikitini,barabarani,ufukweni nk.Kusanya zako hela mkuu..jenga li ghetto lako nunua li usafir la ukweli kama ni kiu tafuta ya kupiga ipite hiv[emoji117].
hawa wanawakee wanateesa akili,tena hawa wa kutafuta online achana nao kabisa.Nina umri kama wako kwa sasa nimeshapitia mengi in short najuta sababu nimerudishwa nyuma kimaendeleo.
Asante sana,umenena kweli kabisaHongera kwa maamuz ya kutafuta mchumba na kuwa atakuwa mke wako , bt mm nakushaur kuwa cc wana jf hatuwez kujua yp mke bora au xo bora .M m naomba umushirikishe Mungu kwanza yy ndy atakuonyesha yp wa kkfaa .
Mkuu kama umesoma vizur nilichokiandika,utakuwa umegundua kwamba sikujielekeza kabisa katika mwonekano wa kimwili, hivyo hukuwa na sababu ya kunitumia picha na kuniuliza,ulichotakiwa kufanya ni kuniunganisha nae tu Mkuuvipi huyu Mkuu atakufaa nikuunganishe
Mkuu unamaanisha nikae tu nitulie bila kufanya jitahada zozote za kutafuta?wew fanya mambo yko tu... mke atakuja mwenyew....
Mkuu kwenye hiyo hadhara unayohadhiri hujapata bint wa kuoa?Mimi ni kijana wa kiume,nina miaka 30. Nimehitimu elimu ya Chuo Kikuu ngazi ya Uzamili. Kazi ni Mhadhiri na ninaishi Mwanza.
Wana JF, natafuta mchumba mwenye umri usiozidi miaka 30 na isiyopungua miaka 24. Dini, rangi, kabila na elimu sibagui ila awe mwenye tabia njema na akiwa ameshajifungua basi wasizidi watoto watatu.
Mimi napenda sana kuangalia muvi,kusoma vitabu, kupiga kinanda na kuimba (Ingawaje sina kipaji), pia napenda sana kusaidia watu wasiojiweza hasa yatima na wajane. Wakuu, udhaifu wangu mkubwa ni kunywa sana pombe ingawaje sivuti sigara.
Kwa hayo machache, naomba kwa mwanamke yeyote ambaye kwa kuzingatia nilichosema,anajua yuko tayari kuwa nami basi tuwasiliane privately.
NB: SIJAOA WALA KUWA NA MCHUMBA MPAKA LEO KWA SABABU YA MAISHA TU.
Nawasilisha.
Ni hadhara mchanganyiko- Wanaume na Wanawake. Sijapata MkuuMkuu kwenye hiyi hadhara unayohadhiri hujapata bint wa kuoa?
au hadhara yako ni ya wanaume tupu?
Jipinde mkuu umpate shemeji kutoka hapo kwenye hiyo hadhara kwani waliomo humu JF ni hawahawa tunaowaona katika ''shughuli zetu'' za kila siku.Ni hadhara mchanganyiko- Wanaume na Wanawake. Sijapata Mkuu
Nashukuru sana kwa ushauri Mkuu ingawaje nadhani ni busara zaidi kama nisipojifunga kwamba ni lazima nipate kwenye hiyo hadhara tu!Minadhani ni vyema zaidi kuwa na uwanja mpana zaidi ili niweze kupata ambaye atakuwa bora zaidi-Ndio sababu na humu JF nimeamua kutupa karata MkuuJipinde mkuu umpate shemeji kutoka hapo kwenye hiyo hadhara kwani waliomo humu JF ni hawahawa tunaowaona katika ''shughuli zetu'' za kila siku.
Hahaha wewe jamaa unanichekesha sana kwanza kwa hivyo vigezo eti kama ana watoto wasizidi watatu ...jamaa hapa kakupa picha unashangaa kwanini haja kuunganisha badala ya maneno mengi ....Mkuu kama umesoma vizur nilichokiandika,utakuwa umegundua kwamba sikujielekeza kabisa katika mwonekano wa kimwili, hivyo hukuwa na sababu ya kunitumia picha na kuniuliza,ulichotakiwa kufanya ni kuniunganisha nae tu Mkuu
Nashukuru sana Mkuukila la kheri
Kigezo cha watoto watatu ni kwa sababu mimi binafsi sioni na wala sijawahi kuona kama watoto wa mwanamke ni tatizo (Ndio maana kuna watoto kadhaa ambao nawalea kama wangu na nikijaliwa uwezo nitaongeza - Sasa kwa nini nimetaja wasizidi watoto hiyo ni kwa sababu ndo napenda iwe hivyo sasa kwa nini napenda hivyo hapo kwa kweli sijui Mkuu )Hahaha wewe jamaa unanichekesha sana kwanza kwa hivyo vigezo eti kama ana watoto wasizidi watatu ...jamaa hapa kakupa picha unashangaa kwanini haja kuunganisha badala ya maneno mengi ....
Unatafuta mke au mtu wa kumtoa kafara ?