Maybe ni :-
1.Asthma- mara nyingi wanakuwa na allergy flani , kwenye familia au ukoo kunakuwa na mtu mwenye allergy, na wanakohoa mara nyingi asubuhi au jioni
2. Post nasal drip syndrome: hawa wanakuwa na kama makohozi yanachuruzika kutoka nyuma kama ya pua kwenda kooni na huwa yananuka
3: laryngopharyngo reflux : hawa wanakuwaga na acid inapanda kutoka tumboni kuja kooni , anakuwa anaiskia ina radha ya uchachu, koo linakauka mara kwa mara , anameza mate mara kwa mara, anaskia kama kuna kitu kooni, anakuwa anakohoa kidogokidogo ili kuondoa tuvitu flani kooni, na mara nyingi kikohozj kinakuwa kikavu na hutokea baada ya kushiba na kwenda kulala
4:rhinosinusitis: kamasi, masikio kutosikia vizuri, kichwa kuuma mbele
5.TB: kwa mwaka mzima bila dawa ingekuwa ni mbaya yaani ungekuwa ushakonda sana na mara nyingi unakuwa na dalili nyingine kama kutokwa jasho usiku na homa , kuvimba tezi,
6.cancer: kwa mwaka bila dawa ungekuwa na hali mbaya zaidi yaani ungekuwa una kohoa na damu, kupungua uzito , kupumua kwa shida na ingekuwa imesambaa sehemu nyingine
7: moyo: unakuwa mara nyingi unapata shida ya kupumua ukilala flat, unasikia moyo unadunda sana, unavimba miguu,
8: dawa : kuna dawa ACEI kama captoril wanatumia watu wa moyo huwa zinaleta kikohozi
9: sarcoidosis
10: COPD
NOTE: ziko nyingi sana ila 5 za mwanzo ndo zinawakuta wengi cha msingi historia yako haijitoshelezi kujua tatizo ni lipi kati ya hayo hapo juu na bado hapo hujafanya kipimo chochote
Hivyo kumwona daktari tena wa magonjwa ya upumuaji au kifua (pulmonologist) na ENT pia ni lazima na haraka kwa sababu magonjwa 5 hapo chini ni hatari sana kama ndio chanzo hivyo yanahitaji kubainiwa mapema na kutibiwa haraka iwezekanavyo kabla hayajafikia hatua mbaya zaidi ingawa kwa jinsi ulivyoeleza ni kama 5 ya juu ndo tatizo ambayo hayatishi sana.