Nakumbuka uchaguzi ule wa mwaka 1995, nikiwa mwaka wa mwisho "under graduate program" ambapo nilikuwa miongoni wa wanachuo ambao tulimsikiliza Mh. Lyatanga Mrema pale Nkurumah Hall akiwa mpeperusha bendera wa nafasi ya uraisi huku akinadi sera za NCCR Mageuzi, na hatimaye kulisukuma gari mpaka geti la UDSM lenye kupakana na Chuo cha Maji, kuelekea njia ya Ubungo.
Nakumbuka, nilikuwa ni mmojawapo wa mawakala ambao tuliteuliwa na chama hiki, ijapokuwa hatukuwa ni wanachama, bali sifa zetu tulikuwa ni wanachuo wenye misimamo thabiti ya kutaka mageuzi. Tullifanikisha kwa ukamilifu zoezi hili ambapo Marehemu Masumbuko Lamwai akaibuka mshindi ktk nafasi ya ubunge.
Pamoja na kuwa ktk kipindi cha mitihani ya kitivo, enzi hizo hatukuwa na mambo ya "collage" chama hili kilitupekeka chaka. Kwa hisia zangu sina imani ya chama hiki chenye "elements" zote za kishushu. Hiki kwa hakika ni "CCM B" toka kwa asili yake na waasisi wake. Wenye kukishabikia na kukumbatia mnalo, hakiaminiki wala kutegemewa kama chama chenye nia ya dhati kuwa "icon of excellence" kwa nia ya kushika dola.
Sent using
Jamii Forums mobile app