g vizy
JF-Expert Member
- Jan 5, 2016
- 907
- 1,000
Habari zenu wana jf wote
Mimi nina mama yangu ambaye ni muathirika wa virusi vya ukimwi kwa kipindi kirefu sasa zaidi ya miaka 10,kipindi cha nyuma kipindi tuko bado wadogo Mimi na dada zangu wawili hatukuwahi kufahamu kuwa mama ni muathirika pengine alishindwa kutuambia kutokana na umri wetu kuwa ni mdogo na hatukuweza kufahamu mambo mengi kama ilivyo ivi sasa
Imepita kama miaka miwili tangu alipotueleza kuwa yeye ni muanga ya gonjwa hili tulilipokea kwa jinsi alivyotueleza na tulimpa moyo kwani siye yeye ambaye kakumbwa na tatizo hilo wapo wengi na wanaishi kama kawaida kwa kufuata ushauri wa daktari juu ya matumizi ya vidonge vya ARV's na hata yeye amekuwa akivitumia pasipo kukosea masharti na wakati mwingine tumekuwa tukimkumbusha avimeze ili asikosee masharti
Sasa hivi limezuka tatizo la yeye kuwa anapungukiwa damu Mara kwa Mara na akienda hospitali wanamwambia awe anatumia sana matunda damu,matembele na dawa Fulani inaitwa hemovit ambayo wanatumia sana wamama wajawazito kuongeza damu pamoja na kutumia hivyo vyote lakini Bado damu yake iko chini sana
Jana ikamlazimu kwenda kuwauliza tena madokta wakamwambia inawezekana likawa ni dawa anazotumia ndizo zinazomfanya damu yake kupungua au virusi kuwa wengi katika mwili wake na kusababisha kupungua kwa damu
Sasa hapo ndo nashindwa kuelewa je virusi kuwa wengi wanausiano gani na kupungua kwa damu na je waathirika waliowengi wanatatizo hili au ni kwa mama angu tu
Asante wakuu naombeni mnijuze na kama mtu anafahamu dawa za asili za kuongeza damu pia anijuze ili nizitafute na kumpatia
GOD BLESS U ALL