Droo ndio imekuwa utamaduni wa Simba Sc kwasasa,wakitoa droo wanshangilia,wakitoa droo wanang'oa viti uwanjani sijajua siku wakifungwa itakuwaje.
Mimi niliacha kushabikia Simba muda mrefu baada ya kugundua kuwa viongozi wa timu wakiongozwa na Rage kuwa ni watu wasio na nia ya kuiendeleza timu bali wpapo pale kujaza matumbo yao na kuivuruga klabu.
Hivi si ndio huyu Rage aliyefungwa jela kw ufisadi?hivi si ndio huyu anayeuza wachezaji bila kuwa na mbadala wa kuziba pengo linaloachwa...yupo wapi mbadala wa Okwi?hivi si ndio huyu anayewaundia zengwe wachezaji ili wawatimue pale wanapoonekana kutetea maslahi ya wachezaji wenzao?...yupo wapi Kaseja?,hivi si ndio huyu Rage aliyeahidi kuwajengea uwanja lakini mwisho wa siku akwakana tena kwa dharau kubwa?.
Sasa mashabiki/wanachama wa Simba kama kama kweli mna hasira na matokeo mabovu ya timu yenu kwanini badala ya kung'oa viti uwanjani mumng'oe huyo Rage na mtandao wake na muweke watu watakaokuwa na uchungu na timu yao,nina amini kuwa huyu bwana Rage angekuwa Yanga wangeisha mng'oa siku nyingi sana maana Yanga hawataki mchezo,Mashabiki wa Simba ni kama makondoo tu maoga kweli,maneno mengi lakini hakuna kitu.
Mnakumbuka msimu wa mwaka jana?mlianza kwa ushindi tu huku Yanga wakiboronga..baadae kibao kikaeguka...Yanga wakabeba ubingwa...hilo linatokea tena msimu huu,mlianza vizuri tena mmeanza kubotonga,safari hii ubingwa Mbeya City au Azam.
Mpaka hapo rage atakapoondoka Simba ndipo nitakaporudi kuishabikia Simba kwasasa wacha niburudike na Mbeya City Fc aka watoto wa jiji.
VIVA MBEYA CITY FC
KUTOKA LIGI DARAJA LA KWANZA MPAKA UBINGWA WA LIGI KUU.
Sasa kama ulishaacha kushabikia Simba kinachokuwasha nini sasa hadi unatoa malalamiko yote hayo, si uwaache wanasimba wenyewe watajua cha kufanya, wewe kama viti vimekuuma ungeongelea swala la viti tu na na mazingira ya penati yaliyosababisha viti ving'olewe.
Ni kweli asilimia kubwa ya mashabiki ambao wanasober mind na wako rational ambao ushabiki wao sio wa mihemuko wamefadhaishwa na kitendo cha mashabiki wa Simba kung'oa viti hata mimi pia nimefadhaishwa na mashabiki wenzangu wa Simba kung'oa viti lakini isiwe sababu ya kuanza kutukana uongozi na watu wengine wasiohusika hasa kwa wewe ambaye ulishachoshwa nao hadi ukahama timu kwa nini usiendelee na yako ya Mbeya City mbona yako mengi tu ulishaona mshabiki wa Simba anashadadia mambo yenu ya Mbeya City ya kupiga magari ya timu pinzani na badala ya kusikitika wewe jana ukawa unawaunga mkono eti si wao walioanzisha fujo mbona hatujaona madhara ya walioanzisha fujo badala yake tumeona madhara ya waliofanya counterfujo?
Viti vitalipwa hata mimi niko tayari kuchangia maana sijafurahishwa na tabia ya kung'oa viti, lakini bado kuna tatizo na TFF, nakumbuka ilikuwa mwaka juzi viti viling'olewa sikumbuki ilikuwa ni mechi gani na baada ya timu husika kutozwa faini badala ya viti kurudishiwa vizuri kwa kufungwa kwa bolt & nut, wao walifunga na binding wire sasa wasije wakarudia na hapa tena.Mi ningekuwa Rais wa TFF hivyo viti vingelipwa na adhabu nyingine Juu.
Ndo maana nikasema kama umesitisha basi acha kuongelea hayo sasa tuache ambao bado tunaendelea na timu tuyaongee, tuongelee yanayotuunganisha kama ujinga wa mashabiki kung'oa viti, ujinga wa mashabiki kupiga magari ya timu pinzani, ujinga wa wachezaji kupiga refa, udhaifu wa marefa katika kufanya maamuzi, lakini kwa mambo yasiyotuunganisha tuache yanayowahusu wayaongee lakini uanweza kutoa ushauri na sio kutukana maana ni sawa na kwenda familia ya jirani badala ya kuwashauri vizuri bila kebehi wewe unaanza kuwakebehi na kuwatukana hata kama ni kweli hawakubali hizo dharau.hahaaa.pole sana mkuu Masuke,kwanza nikwambie nimesema nimesitisha kushabikia simba mpaka Rage atakapoondoka,pia ni wajibu wangu kuwakumbusha mambo muhimu kwani Mbeya city hatuwezi kucheza ligi peke yetu bila kuwa na wapinzani imara.Simba msipoliona hilo la viongozi mtaboronga miaka yote.
VIVA MBEYA CITY FC
KUTOKA LIGI DARAJA LA KWANZA MPAKA UBINGWA LIGI KUU
Ndo maana nikasema kama umesitisha basi acha kuongelea hayo sasa tuache ambao bado tunaendelea na timu tuyaongee, tuongelee yanayotuunganisha kama ujinga wa mashabiki kung'oa viti, ujinga wa mashabiki kupiga magari ya timu pinzani, ujinga wa wachezaji kupiga refa, udhaifu wa marefa katika kufanya maamuzi, lakini kwa mambo yasiyotuunganisha tuache yanayowahusu wayaongee lakini uanweza kutoa ushauri na sio kutukana maana ni sawa na kwenda familia ya jirani badala ya kuwashauri vizuri bila kebehi wewe unaanza kuwakebehi na kuwatukana hata kama ni kweli hawakubali hizo dharau.
Ni rahisi kun'goa viti kwa sababu vinajulikana jinsi vilivyofungwa, kwa kutumia bolt. Ni vigumu kimn'goa Rage kwa sababu hamjui bolt alizofungiwa ndani ya uongozi zilipofungwa; wala hamjui jinsi zilivyofungwa.
Kwanini yanga waweze halafu simba washindwe?