Napata Maumivu makali ya kifua naomba msaada

Napata Maumivu makali ya kifua naomba msaada

Trial balance

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
202
Reaction score
160
Kifua kinaniuma ila sikohoi nikishindilia ngumi napata maumivu makali hata vidole tu nikigandamiza kifuani kifua kinauma chote Nina H paroll positive.
 
Mkuu hao wadudu aka Bacteria wa H-Pylori kwa dawa za hospitali hata utumie kwa mwaka mzima hawawezi kufa hao wadudu Bacteria wa H-Pylori nitafute mimi nipate kukutibia kwa dawa zangu za asili upate kupona maradhi yako.

Nimesha mtibia mtu mgonjwa yupo mjini Zanzibar ametumia dawa zangu na alivyo kwenda kupima wadudu walikufa Vipimo vikaonyesha H-Pylori Negative yaani hakuna tena wadudu amepona na karatasi yake ya Majibu ya hospitali ipo hapo chini angalia. Ukihitaji matibabu toka kwangbu nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia upate kupona maradhi yako.

MAJIBU YA H-PYLORI.jpg
 
Mkuu hio ilikuwa first line treatment na kama umemaliza heligo kit wiki mbili mfululizo na bado unaumwa. Nenda hospitali ukapime tena hao h pylori kama bado wapo.kama hutojali ingia second line treatment( quadruple therapy) na ndo wengi wanapoponea hapo.
Quadruple therapy dosage(10 days-14 days)

bismuth subsalicylate 525 mg+metranidazole 250mg po qid
+tetracyline 500 mg po qid for times a day+ ppi(omeprazole 20mg) twice daily for 10 days.
Kila la heri mkuu.
 
Ni hospital gan mkuu unashauri mtu aende ambapo anaweza pata suluhisho la hawa h pylori sugu?
 
Kifua kinaniuma ila sikohoi nikishindilia ngumi napata maumivu makali hata vidole tu nikigandamiza kifuani kifua kinauma chote Nina H paroll positive.

Pole sana.
Ningependa kueleza kuwa unahitajika kumwona daktari na kusikilizwa upya juu ya tatizo lako. Pamoja na kuwa na hao H.Pylori uwezekano kuwa na tatizo jingine pia upo.

H.pylori huweza kupelekea kuumizwa kirahisi kwa njia ya chakula. Hii huweza kuleta hali ya michubuko/gastritis au kuwa na vidonda vya tumbo.

Si kila mwenye H. Pylori positive ana vidonda vya tumbo na si kila mwenye vidonda vya tumbo basi ana H. Pylori.

Mambo ya kuzingatia:
1: H. Pylori huweza kutibiwa na kupona hospitali. Ila, usitumie dawa za kuondoa H. Pylori na kwenda kupima ndani ya si chini ya mwezi mmoja. Kwani, vichocheo vilivyotolewa na mwili huwa havijaisha mwilini. Pia, usiende kupima H. Pylori wakati unatumia dawa za kukontrol acid na gesi kwani huweza kuingilia mfumo wa kipimo na kufanya kuwa positive. Kaa siku saba bila kumeza dawa za acid na gesi ndipo uende kupima H. Pylori.

2: Unapomaliza dozi ya H.Pylori ni vyema kuendelea na dozi ya dawa za kukontrol acid kama wewe uliambiwa una gastritis au vidonda vya tumbo. Kwa muda gani, hutegemea na hali yako, daktaria takuongoza kwa hilo.

3: Kipimo cha kuaminika cha H. Pylori ni kile cha kupima kupitia CHOO TU. Na si zaidi ya hapo. Au sample iliyochukuliwa wakati wa endoscopy tu.

4: Si kila mwenye gastritis au vidonda vya tumbo anahitaji kutumia Heligo kit au antibiotics.

5: Zingatia maelekezo yanayoambatana na tiba yako. Ule au usile nini. Ufanye au usifanye nini.

Tiba njema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom