Nyakwaratony...BMI, kipimo kinachokuonyesha simply how fat you are by relating your weight by height, kwa uzito huo wa kilo 62 na urefu wa futi 5'6 uko kwenye 'normal weight'...yaani uzito wako unaendeana na urefu wako. Hiyo inakupunguzia risk ya magonjwa ya moyo na kisukari huko baadae. Ukipandisha mpaka kilo 68, utakuwa borderline overweight, taratibu unajongea kwenye risk hizo. Mimi nakushauri maintai uzito wako hapo.
Ni kawaida watu kuona una magonjwa au unadhoofu kwa kupungua uzito, na vile vile kuona eti ndio una afya na maisha yamekuwa mazuri unaponenepa...sasa wewe inabidi uchague, unaishi kufurahisha watu au kufurahisha nafsi yako. Kama nafsi yako unafurahi na unakuwa na self confidence kuwa kibonge....sawa, lakini ujue gharama yake ni kujiweka katika risk ya magonjwa yasiyoambukiza.