Naombeni ushauri

mkemiamkuu

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
355
Reaction score
284
Habari wana MMU, ni mara yangu ya kwanza kuomba ushauri hapa jf lkn kwa hili naombeni mnisaidie.

Nilikuwa na girlfriend wakati nasoma chuo na tulipendana sana, tukapoteana ktk harakati za maisha na kila mmoja akapata mwenza wa ndoa. Mwezi uliopita wa 11 nikaona call baada ya kupokea nikakuta ni huyo dada, tukaanza kuwasiliana kawaida kabisa, siku moja akanipa story kuwa toka aolewe yapata miaka minne sasa hajapata mtoto na walipochunguzwa hosp ikabainika mumewe ndo mwenye tatizo hawezi kuzalisha. Wakakaa chini na kukubaliana ili kutunziana heshima huyu dada statute mwanaume alale nae ili apate ujauzito.

Sasa ndo huyu dada kaamua kunitafuta kwa udi na uvumba na kuniomba mm ndo nimpe ujauzito. Mimi nina mke na mtoto mmoja na sipendi kumkwaza mke kwa hili.

Huyu dada anaomba sana nimsaidie maana pia anasumbuliwa na tumbo na kaambiwa akizaa halitamsumbua tena. Ushauri wenu wana MMU nimsaidieje huyu dada.
 
Ikiwa ni udhauri kwako wewe usithubutu kufanya hilo., ushauri kwa huyo dada kama anataka kweli kutunza heshima azae na mtu asiemjua na wala huyo mwanamme asijue kua amempa ujauzito
 
Ikiwa ni udhauri kwako wewe usithubutu kufanya hilo., ushauri kwa huyo dada kama anataka kweli kutunza heshima azae na mtu asiemjua na wala huyo mwanamme asijue kua amempa ujauzito

Hii ni sawa au akafanye artificial insemination.
 
Nafikiri Wewe kutoka nje ya ndoa yako utakua unafanya jambo la hatari sana juu yako na familia yako na imani yako.

Sio kitu rahisi ujue damu yako iko mahali halafu upretend sio yako, kama sio leo ni kesho lazima utaenda kumdai tu mwanao tena kwa nguvu kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiri (wazee wenzangu wanajua damu ilivyo nzito). Mambo sio marahisi kama unavyotaka kufikiria.

Pili haitaishia hapo, itakuwa ndio mchezo wenu na sio kwamba utamtunzia siri huyo mume bali ndio utamharibu zaidi. Utajikuta mmezaa wa pili na wa tatu pia. Hapo utakua umeshaharibu ndoa yako na yao pia. Watu wawili wakiwa wanajua kitu hakiwi ni SIRI labda afe mmoja wao... namaanisha hakuna Siri nje ya mtu mmoja. mkishazidi mmoja sio siri tena hio. Si unaona hata sisi tunajua? Unafikiri haiwezekani mumewe akawa yuko humu? SO HAMNA SIRI APO.

Tatu, usijisikie kama una wajibu wa kumsaidia, wala hapo humsaidii utakua unamuharibia sana, trust me. Ila mtu akiitazama kwa hisia hii habari hataelewa nachoonesha hapa. Stick with your wife and your wife only.


Nne; Nafikiri mshauri atafute ''second opinion'' kwa wataalamu wengine ili kujua uwezekano wa kupata mtoto ukoje kama atarekebisha life style yake maana kuna uhusiano wa moja kwa moja wa maisha tunayoishi siku hizi na uwezo wa kupata mtoto. Pia maombi ni muhimu sana, mshauri pia juu ya hio habari ya Maombi. Nothing is impossible before God.
 
Mwambie eende hospitali, wampandikize mbegu ashike mimba
 
Nashukuru ndugu zangu kwa ushauri mzuri mnaonipa
 
Ikiwa ni udhauri kwako wewe usithubutu kufanya hilo., ushauri kwa huyo dada kama anataka kweli kutunza heshima azae na mtu asiemjua na wala huyo mwanamme asijue kua amempa ujauzito

Sasa hili litawezekanaje alale na mtu asiemjua?
 
Mshauri akiwa katika siku zake za kushika mimba, aende mkoa wa mbali na anapoishi, akifika huko, aende klabu, halafu ajirahisishe kwa mwanaume yoyote wagegedane, asubuhi yake arudi kwake bila kuchukua mawasiliano yoyote ya mgegedaji. Hapo atakuwa kapewa ujauzito na mtu ambaye hawezi kusumbua siku za mbele.
 
hivi bado watu wanatumia local ways like that

si afanye artificial insermination..period
 
Aende India atapata tiba nzuri.........
 
Na kwanini uwe wewe asiwe mwengine asokua na mtoto wala mke? nendanae kwa mumewe mkae nyie wote watatu kama kweli utajua hapo na kama uzushi wa huyo mwanamke utajua hapo,jengine mshauri aende India kuna hospiatal wanafanya hizo kazi kwa bei poa na nisalama rafiki yangu amefanya sasaivi ana twins wana miaka m4.............
 
msaidie mwenzio, ili ujue ukwel, kama na wew mtoto aliopo ndani si wa kwako? msikilize, kwan nan atajua, japo damu nzito kuliko maji
 

Duh!Hahahaha!!Jamaa naye akiwa hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba itakuwaje sasa hapo mkuu
 


Wakuu nafikiri huyu dada kamchagua mkuu mwenzetu sababu hataki kuzaa na mtu ilimradi tu. Anataka kuzalishwa na mtu anaye mfahamu kitabia na asili yake

Mkisema sijui aende club ajirahisishe kwa Mwanaume yoyote anaweza kuja kujifungua mtoto wa ajabu Maana hujui historia ya huyo mwanaume. Wengine wana matambiko na magonjwa ya ukoo kwahiyo ukiokota tu mwanaume mtaani unaweza ishia pabaya

Ushauri mzuri hapa ni artificial insemination. Hata South Africa Wanafanya sio mpaka India japo nahisi India inaweza kuwa cheap zaidi. Lakini Pia mme wake atakuwa na amani zaidi kuliko hiyo Njia wanayotaka kufanya sasa mbeleni itakuja kumnyima amani mme wake,hata kama una shida kugegedewa mke kunauma

Mleta uzi tafadhali usije mgusa huyo dada,utakuwa humsaidii bali uta hatarisha ndoa zenu. Mpe huo ushauri
 

Thanks ntalifanyia kazi, nahisi hili litamsaidia
 
Sasa ndo huyu dada kaamua kunitafuta kwa udi na uvumba na kuniomba mm ndo nimpe ujauzito.


Ushauri wenu wana MMU nimsaidieje huyu dada.

Huyo akifanya hivyo ,hapo itakuwa hamna ndoa tena aisee!
Cha muhimu wakaadapti mtoto mchanga kwenye vituo vya kulelea watoto waliotelekezwa na yatima.
 
Kweli ni ushauri mzuri ila sina uhakika kama umezingatia gharama , hiyo kitu siyo chini ya Million 20 na inaweza isiwe successful mpaka ujaribu zaidi ya Mara moja.
Hata hapa bongo inafanyika
 
Huyo akifanya hivyo ,hapo itakuwa hamna ndoa tena aisee!
Cha muhimu wakaadapti mtoto mchanga kwenye vituo vya kulelea watoto waliotelekezwa na yatima.

Hili nilijaribu kumwambia lkn akasema shida ni kwamba hata mume wake hataki ndugu jamaa wasijue kuwa hana uwezo wa kuzalisha so anataka watu waone wife akiwa mjamzito ili waonekane wako fit
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…