martinezmarty
JF-Expert Member
- Apr 17, 2017
- 316
- 506
COPD mara nyingi huwapata watu wa 50+ lakini mazingira ya mgodini ni risk factor.Asante sana, naanza kama ifuatavyo,
1. Sigara nilivuta kwa muda wa wiki mbili hizi ni za madukani club sport, master sports n.k, pia bangi nilitumia mwaka 2014 baada ya kumaliza chuo, ila baada ya bangi kunikataa niliacha mwenyewe na kuamua kuachana na uvutaji wa aina yoyote mwaka huo huo. Nilikuwa nimeasi kanisani nikarudi kutubu, mpaka sasa situmii sigara ya aina yoyote tangia mwaka 2014.
2. Nafanya kazi mgodini. Mwanzoni nilikuwa naenda sehemu za kuchimba almasi na sehemu hizo zina vumbi sana, nimefanya kazi kama miezi 9. Baada ya hapo nikaacha na kurudishwa ofisini, ila nimeacha kazi na kifua kilikuwa kinanisumbua siku hadi siku.
Nakumbuka nilikuwa na desturi ya kunywa maji sana usiku, ili niwe macho kulingana na kazi niliyokuwa nafanya, ilifika sehemu nilipoacha tu kunywa maji kwa wingi ndio tatizo likanipata mpaka sasa tangia mwaka jana mwezi wa (11). Pia mimi tangia udogo wangu nilkuwa nikikimbia naenda na pumua kwa kasi mpaka sasa ni hivo hivo tu.
Mazingira ya mgodini kiukweli vumbi ni ya kutosha pia baridi lina msimu kuanzia mwezi wa sita huwa kali na kweli lilinisumbua sana, nilikuwa sipendi kuvaa makoti nikiogopa kusinzia kazini.
3. Umri wangu miaka (25).
Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia akafanye chest X-ray na lung function test. It might be helpful katika kujua what's up with him, as far as Pneumoconiosis is concerned.COPD mara nyingi huwapata watu wa 50+ lakini mazingira ya mgodini ni risk factor.
Anza vipimo vya lung function kwanza.
Ni vigumu kwangu kujua gharama mkuu.Hebu naomba unisaidie kujua gharama, ili nijue najipanga vipi
Mkuu tuulize wote gharama humu tunaweza kupata msaada. Kwa wanaofanya kazi hospitali au walioguza ndugu na jamaa. Ukipata clinic nzuri ya respiratory diseases utanufaija sana.Hata kiasi cha kuanzia huwezi fahamu
Asante sana, nimejifunza kitu. Kuanzia sasa hiriki hazitakosekana kwangu, nitatumia mara kwa mara kwa ajili ya afya yangu.Wengi hatuna uelewa wa COPD, kijijini kwetu wagonjwa wa kifua cha mshipa walipewa chai ya iliki. Iliwasaidia kutibu kifua. Baada ya kugundua kuwa iliki ni natural antibiotic, nikafahamu babu zetu walikuwa na maarifa sana. Ukipika maandazi ukiweka iliki ina inhibit fungal kwa muda mrefu kuliko maandazi yasiyo na iliki.
Asante kwa ushauri wako na Mungu akubariki sana.Dodoma kuna Dispensary moja ipo Majengo Sokoni, ni ya Wachina wanatibu vizuri sana. Kuna ndugu yangu alikuwa anasumbuliwa na tatizo kama lako, wana mashine nyingi za kutafuta tatizo na hatimaye kulitibu