Ushauri: Amesema hahitaji mahusiano wala kuolewa na mimi, ila bado nampenda

The Hidden

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
246
101
Tangu niwe na mpenzi wangu ni miaka miwili sasa imekatika, tumekuwa tukigombana mara kadhaa na mengine makubwa zaidi ya hili lilotokea sasa, yaani ilikuwa juzi nilipokutana na msala fulani kazini na nikamwambia huyo mpenzi wangu kwamba nilitegemea kwa msala ule mdada ninayefanyanaye kazi ofisi moja angenisaidia kwasababu tulifahamiana zamani sana kabla ya kukutana hapo kazini tena lakini nashangaa ndiye aliyenikandamiza kabisa.

Huyu mpenzi wangu anawivu sana, kitendo cha kumwambia hivyo tu alipanic na mimi nikamwambia "huo wivu ni wa kipuuzi" kusikia hivyo akapanic zaidi na kukata simu, baada ya hapo nilimchunia kidogo kwa siku tu japo si kawaida yangu, baada ya hapo.

Nikamtafuta kwa simu kwa sababu sasa tuko mbali kikazi(mikoa tofauti ) lakini hakupokea simu ila akatuma SMS kwamba"siku nzima umenisahau sababu ya huyo mdada ndo unanitafuta sasa, sihitaji simu yako " baada ya hapo nilipiga simu sana hakupokea mpaka hapo jana alipopokea na kusema haitaji mahusiano tena na haitaji tena kuolewa ila tubaki marafiki tu huku akikumbushia mambo mazito sana nilomkosea huko nyuma lakini kwa mbinde tukarudiana.

Wakuu, kauli yake imenichanganya na anaonekana hajali. Naombeni ushauri wenu sababu bado nampenda, na hata yeye tukiwa katika amani alionesha kila dalili za upendo lakini anaonekana ni mtu mwenye maamuzi magumu.
 
Alikuwa anatafuta sababu na keshaipata
Muache aende husipoteze muda wako
 
huyo yupo na wewe either akipoteza muda ili mtu wake mwengine amuoe au kuna mtu anamshika masikio huko alipo

kuna taarifa mbaya zitakuja kwako

maana imeandikwa mtu apendaye hulilinda na kulipigania penzi lake
malavidavi 6:7-9
 
Pole mkuu,

Nashauri ianzishe course ya mapenzi katika taaluma zetu huko vyuoni maana wanadamu wanafaulu course zote lakini wakifikia kwenye hili neno MAPENZI wanakwama!

brain is the beautiful part of the body.
 
huyo yupo na wewe either akipoteza muda ili mtu wake mwengine amuoe au kuna mtu anamshika masikio huko alipo

kuna taarifa mbaya zitakuja kwako

maana imeandikwa mtu apendaye hulilinda na kulipigania penzi lake
malavidavi 6:7-9
hili ni agano lipi, jipya au la kale?

brain is the beautiful part of the body.
 
Tangu niwe na mpenzi wangu ni miaka miwili sasa imekatika, tumekuwa tukigombana mara kadhaa na mengine makubwa zaidi ya hili lilotokea sasa,
Kama hamuwezi elewana si kila mtu ashike njia yake? Kwani watu wameisha Duniani? Kwani lazima umpende huyo huyo?
 
Kuna wakati nilidhani kama unavyodhani nikamchukua msichana mwingine chapchap alipogundua alilia mbele za watu kama mtoto, coz nilimpenda sana nikaachia ugenini nikaendelea naye, sasa sijui maamuzi yake huwa yanalenga nini mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Mwanamke anayekupenda hata ufanye makosa makubwa kiasi gani atakusamehe tu maana wewe ndo kama pumzi yake na furaha yake. Lakini ambaye hakupendi haoni ajabu kukupoteza.
 
Tangu niwe na mpenzi wangu ni miaka miwili sasa imekatika, tumekuwa tukigombana mara kadhaa na mengine makubwa zaidi ya hili lilotokea sasa, yaani ilikuwa juzi nilipokutana na msala fulani kazini na nikamwambia huyo mpenzi wangu kwamba nilitegemea kwa msala ule mdada ninayefanyanaye kazi ofis moja angenisaidia kwasababu tulifahamiana zamani sana kabla ya kukutana hapo kazini tena lakini nashangaa ndiye aliyenikandamiza kabisa. Huyu mpenzi wangu anawivu sana, kitendo cha kumwambia hivyo tu alipanic na mimi nikamwambia "huo wivu ni wa kipuuzi" kusikia hivyo akapanic zaidi na kukata simu, baada ya hapo nilimchunia kidogo kwa siku tu japo si kawaida yangu, baada ya hapo
nikamtafuta kwa simu kwa sababu sasa tuko mbali kikazi(mikoa tofauti ) lakini hakupokea simu ila akatuma msg kwamba"siku nzima umenisahau sababu ya huyo mdada ndo unanitafuta sasa, sihitaji simu yako " baada ya hapo nilipiga simu sana hakupokea mpaka hapo jana alipopokea na kusema haitaji mahusiano tena na haitaji tena kuolewa ila tubaki marafiki tu huku akikumbushia mambo mazito sana nilomkosea huko nyuma lakini kwa mbinde tukarudiana . Wakuu, kauli yake imenichanganya na anaonekana hajali, naombeni ushauri wenu sababu bado nampenda, na hata yeye tukiwa ktk amani alionesha kila dalili za upendo lakini anaonekana ni mtu mwenye maamuzi magumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • FB_IMG_1500616419806.jpg
    FB_IMG_1500616419806.jpg
    26.9 KB · Views: 26
Kuna wakati nilidhani kama unavyodhani nikamchukua msichana mwingine chapchap alipogundua alilia mbele za watu kama mtoto, coz nilimpenda sana nikaachia ugenini nikaendelea naye, sasa sijui maamuzi yake huwa yanalenga nini mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
inshort bro huyo msichana umemuumiza sanaa,kachoka sasa,, too much is harmful broo,, and people change when they loose interest wth you
 
Back
Top Bottom