Naomba update za escrow

Mudawote

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
11,570
Reaction score
16,017
Great thinkers ndiyo narejea home, je kunani leo kuhusu escrow? Je bibi karuhusu mjadala?
 
Leo James Mbatia aliomba bunge lisitishe shughuli zote za bunge zilizopangwa kufanyika leo ili wajadili kuibiwa kwa nyaraka za CAG ndani ya ofisi ya Spika. Lakini Spika Makinda alikataa kwa kusema kuwa jambo hilo lipo polisi tayali. Mnyika na Lissu nao walijaribu kumshawishi spika kuhusu jambo hilo, lakini spika aliendelea kuweka ngumu. Na jioni hii bungeni Werema aliomba watu wanaomchafua kwenye mitandao waache mara moja kwa maadai kuwa tusubiri report ya PAC hapo jumatano. Pia Werema alitumia fursa hiyo kumpongeza Kafulila kwa kufunga ndoa. Ndo hayo makubwa yaliyojili mkuu...Mengi zaid tusubiri Jumatano
 

Asante Tuwaseme kwa info. Ama kweli bibi lazima abane. Maana issue hiyo inaonesha kugusa wengi.
 
Last edited by a moderator:
AG Werema leo anampongeza Kafulila?!

Si huko siku za nyuma, alidiriki kumwita Tumbili na akatishia kunyofoa kichwa chake?

Ina maana leo ameanza kutafuta 'huruma' kwa Kafulila kwa kuwa ameona zimebaki less than 24 hours, ambapo mbivu na mbichi zitaanza kujulikana?

Na hapo ndipo watanzania tutakapojua ni nani hasa kati ya Werema na Kafulila, ambaye ndiye tumbili original!
 
Ndo viongozi wetu hao. Werema anatoa pongezi kwa mambo ya ndoa, anashindwa kumpongeza kwa issue ya escrow. Unafiki tu huo.!
 

= tayari
= yaliyojiri
 
= tayari
= yaliyojiri

Huu si muda wa ku quote watu unless na wewe uwe ni mmoja wa wachumia tumbo mlozoea kujilimbikizia mali.Hili swala ni lazima lipate ufumbuzi kwa lugha yoyote haijarishi watu wanakosea namna ya kuandika au vipi kwetu mtu huyo hajatukosea kama mijizi inayotukosea kutuibia mabilioni,tena wewe bibi faiza foxy uvuruge huu mjadala usiuvuruge lazima watu hawa wawajibishwe hela zetu zirudishwe.wakuu endeleeni kutoa maoni yenu achaneni na hivi vizee vinavyotumiwa kumsafisha mtu alobeba fuko la m.a.V.I
 

= haijalishi
 
Tumeacha hoja tunavamia lugha. Mtaalamu wa Kiswahili FaizaFoxy changanua sentensi hii kwa njia ya matawi "Wali wale walikula wali kwa liwali wa Liwale"
 
masingasinga na wageni jamii ya kiarabu wanaipenda sana ccm na ujangili wake! na haya ndio maajabu ya tanzania na wahindi wake wote ni kupiga deal kwa kwenda mbele
 
Tumeacha hoja tunavamia lugha. Mtaalamu wa Kiswahili FaizaFoxy changanua sentensi hii kwa njia ya matawi "Wali wale walikula wali kwa liwali wa Liwale"

=Wari

Kwi kwi kwi teh teh teh
 
Tomorrow we unmask falsehood, and bring truth
to light. Mungu ibariki Tanzania.
 
WAZIRI wa Nishati na Madini,Prof.Muhongo, amehusishwa na wizi wa nyaraka zenye ripoti ya CAG kuhusu ufisadi wa Sh.bilioni 300 katika akaunti ya Escrow
 
Na huyo bibi bomba kumbe ni mmoja wa wanufaika!. Kalamba us dollar one million. Atazifanyia nini?. Tuone kama na hili atachomoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…