Naomba nitolewe ushamba katika hili...

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,651
Reaction score
4,758
Hizi namba za kwenye switches za fridges zinamaanisha nini exactly...

Mfano 1 mpaka 5...ina impacts gani kwenye utendaji kazi wa fridge na ulaji wa umeme?
 
Zile namba zipo kwene kidude kwa kingereza kinaitwa fridge’s temperature dial(kwa kiswahili watanisaidia) ambacho kinaonyesha refrigerant power. Sasa basi, Namba inavyozidi kuwa kubwa na ubaridi ndio unaongezeka, maanake ukiweka kwene tano ubaridi ndio unakuwa hatari. Kuhusu kula umeme hapo ntasaidiwa na mafundi umeme, sijui sana umeme...


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
zile namba ni za thermostart ambayo ni biometric switich kazi yake ni kuendesha mfumo wa jotoridi wa ndani wa friji
Switch hiyo imeundwa sambamba na Compressor ikifika kiasi cha jotoridi ambalo umeruhusu eidha namba 3 au namba 5 basi thermosensor uipa taarifa thermostart na kuizima compressor mpk ifike chini ya ubaridi ule uroruhusu
kwa maana nyingne km ukiweka namba ndogo compresa itazima lkn itawaka baada muda mchache thermistart ikipewa taarifa uhitaji wa ubaridi nayo itaipa umeme compressor frij itawaka
lakini katika vitu vya winding na ulaji wa umeme,zima washa zima washa vinakura umeme zaidi na ukipiga full speed umeme unakwenda zaidi pia
hvyo naweza sema haipunguzi wa haili umeme mwingi kwa kuwa compressor winding yake aina speed regulator yenyewe ikiwaka mwendo mdundo km pasi uweke speed namba 5 au namba 1 kiasi cha umeme ni kilekile kinachoenda
kama compressor 250watts basi pale inapoanza fanya kazi inaenda yote

ukitaka kusave umeme wa friji jizoeshe kuwasha friji Asubuhi ifanye kazi halafu jioni zima km kuna vitu vya kuharibika basi iwashe kuanzia saa 6 usiku
ila kusave umeme jenga utaratibu wa kuwasha Asubuhi izime jioni saa 12 au 11 utasave sana Unit zako za umeme mana balaa la saa 1 usiku umeme huu wa bongo na vitu vya winding utaumiza Unit zako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona mtu anahaha zima washa ujue hali yake kimaisha ni mtu wa kulazimisha maisha. Hajafikia wakati wa kumiliki fridge ila analazimisha. Ni bora tukajitathimini kwanza kabla ya kujiingiza katika maisha ya hali ya juu. Mfano ulmwingine unamuona kijana anamiliki gari mara paaa unamkuta kwenye daladala unamuuliza Bro vipi, anajibu nasevu mafuta!!!! Huyo hajafikia kiwango cha kumiliki gari bali analazimisha kuwa na gari bora angenunua tu baiskeli
 
Hizi namba za kwenye switches za fridges zinamaanisha nini exactly...

Mfano 1 mpaka 5...ina impacts gani kwenye utendaji kazi wa fridge na ulaji wa umeme?
1 to 5 inamaana 'warm' to 'coldest' setting

Friji nyingi zina range ya 0.5°C - 4°C ambapo 4°C ni joto ukilinganisha na 0.5°C (ubaridi)
so hiyo dial 1 mpaka 5 actually ni 4°C na 0.5°C respectively

i.e
Dial 1 correspond to 4°C (joto)
Dial 5 correspond to 0.5°C (ubaridi)

Dial 2, 3, 4 ni simple math, ni any temperature range between 4°C mpaka 0.5°C.

Kuhusu kula umeme:
Actually fridge temperature dial control haili umeme.

Compressor ikizima hapo haili umeme
Ukiset dial (1-5) haili ememe wowote
Umeme unaliwa na compressor regardless na dial setting.

Dial ni kama air valve control just una control kiasi cha air refregerant iliyokwisha zalishwa na compressor ipite kwenye freezer

Ni Sawa na kutumia pump inayokula umeme unit 2 kujaza tank. Halafu uzime pump then Una control speed ya maji Kwa koki kwenye tank. Maji ujazo yanajulikana, unit 2 zimeshaliwa na pump, ku control speed ya koki kwenye tank hakuli umeme wowote.
Pump= compressor
Koki= temperature dial control
 
namba 5 inaleta ubaridi fasta, umeme unaenda mwingi
namba 1 ubaridi mdogo, so umeme unaenda mdogo
 
Yaani kwa ufupi ukiona fridge yako haigandishi vizuri au inachelewa kupata ubaridi, ongeza namba toka ndogo kwenda kubwa na yapo utapata ubaridi wa hatari kwenye fridge yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NIMESHIBA MAELEZO YAKO... BASI NILIDHANI INA UHUSIANO NA ULAJI WA UMEME.
 
Na je vipi kuhusu kiwango cha watts na ulaji wa umeme?

Naomba ufafanuzi tafadhali...
 
Na je vipi kuhusu kiwango cha watts na ulaji wa umeme?

Naomba ufafanuzi tafadhali...

Simple Thermodynamic cycle Tu:

Ulaji wa umeme wa friji inategemea na factors kadhaa
1. Constant factor
2. Variable factors/miscellaneous usage

1. Constant factor
Hii ni Electrical power rating ya friji kuonesha friji/compressor inataka Power kiasi gani ili iwe ON bila kuweka chochote ndani.

Mfano 130Watts, etc

Watts = ukubwa wa friji

Kwahiyo ukiwasha friji yako bila kuweka kitu ndani inakula 130W Kwanza,
Ikiwaka say Kwa masaa 10 bila kitu ndani inakula 130watts x10hrs= 1.3kWh units. Hapa usihesabu compressor cycles

2. Variable factors/compression cycles

Hapa ni power ya kua ON + factors mbali mbali zinazofanya umeme ulike Sana
Mfano
-kufungua mlango wa friji
-friji ikiwa na Ka uwazi cold air ina leak
-poor evaporation/fault
-compressor fault
-etc

Mfano
Ukifungua mlango wa friji ikiwa inarun
Cold air inapotea na hot air inaingia ndani ya friji hii hufanya compressor ichukue kiwango kikubwa zaidi cha umeme kukeep temperature ileile iliyopotea. Ndiyo mana friji za LG baadhi zina kioo yani unaangalia cha kuchukua kabla hujafungua mlango for energy savings, inaloose compression

Sasa hii loss + power ON loss = cost

Mfano2:
Ukiweka chakula cha 40°C compressor itakula umeme zaidi kuzalisha low temperature refrigerant ku cool hii 40°C mpaka dial set point, ambayo ni tofaut na aliyeweka chakula cha 20°C itakula umeme chini ya aliyeweka 40°C for the same dial setting. Thermodynamic cycle tu hapo

The colder the system, the higher the supply energy needed to keep that lowest temperature and make system colder, and vice versa.
 
sio kweli
 
BABA SALUTE KWAKO KWA ELIMU...

JE MFANO NATUMIA FRIJI YA MR UK... WATT 300 NDOGO MLANGO MMOJA...NIFANYE NINI ILI NISAVE UMEME KULIKA. .. JAPO INAJIZIMA NA KUJIWASHA? JE HIYO KUJIZIMA NA KUJIWASHA INA MSAADA WOWOTE KWENYE UMEME KULIKA?
 
BABA SALUTE KWAKO KWA ELIMU...

JE MFANO NATUMIA FRIJI YA MR UK... WATT 300 NDOGO MLANGO MMOJA...NIFANYE NINI ILI NISAVE UMEME KULIKA. .. JAPO INAJIZIMA NA KUJIWASHA? JE HIYO KUJIZIMA NA KUJIWASHA INA MSAADA WOWOTE KWENYE UMEME KULIKA?
Yes ina msaada Sana

Ukiset temperature dial say number 3 or any desired °C set, compressor inafanya kazi kuachive hiyo Temperature set if reached sensor(thermostat) itazima compressor/umeme...joto likipanda tofauti na already set point inajiwasha tena ku compensate hiyo change. Ikifika tena set point sensor inazima compressor, etc.

Hii inasave umeme sababu kama umeset Temperature na hiyo Temperature imefikiwa basi compressor izimwe Kwa muda Tu maana cold gas ndo itakua ina circulate mpaka tena joto lipande.

Ni automatic.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…