Ukijibiwa mkuu na mimi nitabata suluhisho mimi ikifika usiku nawashwa mwili wote nikijikuna natokea malengelenge ajabu asubuhi , mchana nakuwa sawa ila ilifika usiku ndio kasheshe inaanza
Kama mko Dar es alaam area, nendeni kibaha, pale usawa wa minzani Zamani,kuna hospitali inaitwa mad wely, sina hakika kama jina la hospitali, kama nimeliandika kwa usahihi.
Ila ukifika eneo tajwa, hospitali ipo upande wa kushoto, ukitokea Dar.
Pole sana, jaribu kutafuta tiba japo na mimi nasumbuliwa sana na muwasho wa ngozi kila ninapotoka kuoga au ikifika jioni.na pia nikijikuna ngozi inavimba km mtu alipigwa fimbo.
Mwenye kujua dawa atusaidie.