Kwa taarifa yako, ni ahadi kama hizo za kurejesha nyumba za serikali, kufikisha mafisadi ikiwa ni pamoja na mama mkuu mahakamani ndizo zimefanya muungwana na washkaji zake kuanza kukazania wimbo wa "mtu" anayetaka kuingia ikulu hata kwa kumwaga damu na kukanyaga maiti za wa-TZ kama ngazi. Inatisha! Wakati mwingine kauli za kuwarudi wakosaji zinawafanya walioko madarakani kuanza kuungana na kujiandaa kwa maafa. Kuna wakati nilifikiri ingekuwa vyema Dr. Slaa asiwe specific na matishio yoyote bali ayaweke kwenye mkakati wake wa kuongoza nchi. Kauli ya Shimbo si bure. CCM hawako tayari kupoteza maslahi waliyojikusanyia.