Nani bado anakumbuka Mambo Haya?

Sodoku Myebusi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,320
Reaction score
3,009
Likizo imekuwa na mambo mengi moja wapo ni kuwa karibu na watoto. Mtoto wangu amekuwa akinitaka nimtengenezee vitu hivi ambavyo binafsi nmeshasahau.
1. Box la karatasi
2. Boat ya karatasi
2. Plane ya karatasi

Kipindi cha nyuma nilikuwa nafahamu namna ya kukunja kupata umbo husika.kwa sasa ni miaka mingi imepita kiasi nmeshasahau.nmejaribu kuangalia youtube. Nmekuta namna wanavyofanya na kuweza kutengeneza

Lakini wao utengenezaji wao si mrahisi kama ambavyo nlikuwa nafahamu mimi before.kuna utofauti mkubwa sana.

Nani anakumbuka namna ya kutengeneza maumbo haya kwa karatasi?zamani ilikuwa ni michezo yetu tuliokua miaka hiyo.
 
Importations za midoli na vifaa vingine vya kuchezea watoto zingewekewa restrictions kali toka kipindi cha Mzee Mwinyi ungekuta leo hii watoto wamesha develop hivyo vitu kua na ubora wa juu zaidi

Tuliporuhusu kuingia kila kitu imesababisha kuua zile akili za innovation kwa watoto na vijana wa taifa hili. Wakati wa Mwalimu Nyerere watoto walikua wanajitengenezea vifaa vyao vya kuchezea kwa kutumia locally available materials na walikua wakitengeneza with state of the art kuanzia magari ya watoto, midoli n.k
 
Ni kweli ujio wa midoli kutoka nje imeharibu vipaji vya watoto.

Nakumbuka miaka hiyo ya tulikuwa tunatengeneza wenyewe magari ya michezo hile mazuri sana, unatia na spring kabisa, mm nakumbuka nilisota kwa rafiki yangu hadi nikajua kutengeneza ndege then tunaweka na mota Kabisa..

Ulikuwa ubunifu wa hali ya juu kabisa watoto wa siku hizi wamekosa raha hizi.
 
Siku hizi kina Junior wanakaa ndani wanacheza Playstation, Xbox... nk. watajulia wapi vitu kama hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…