Kuna wimbo mmoja naupenda sana lakini sina bahati ya kuujua wala kuwa nao!! Ni wa kitambo kidogo nimekuwa nikiusikia kwenye maredio tu, jina lake sijwahi kulijua.
Wimbo sijui umeimbwa na nani ila amemshirikisha Banza Stone na hata sehemu ninazozipenda zaidi ni zile alizoimba Banza!
Banza anaimba hivi "Hata ukoo sina, sina ndugu wa damu. Wala kabila sina udini, sijui mmakonde!! Au msukuma, sijui mmasai au mluguru"
Kuna bridge ya kimchiriku Banza anaimba "Nalia lia mama oooh, uko wapi mama oooh, nalia lia mama ooh! Uko wapi mama oooh!! Nataka kucheza eeh nataka kudekaa!! Kucheza eeeh! Nataka kudekaaa!!"
Kama kuna mtu anao, au anaujua jina mnipatie niweze kuupata, wimbo unanikuna sana huu. Msaada wenu please wana JF
jina la wimbo limenitoka ila ni utunzi wake Banza Stone alipokuwa na bendi ya TOT mwaka 2002.
Kuna wimbo mmoja naupenda sana lakini sina bahati ya kuujua wala kuwa nao!! Ni wa kitambo kidogo nimekuwa nikiusikia kwenye maredio tu, jina lake sijwahi kulijua.
Wimbo sijui umeimbwa na nani ila amemshirikisha Banza Stone na hata sehemu ninazozipenda zaidi ni zile alizoimba Banza!
Banza anaimba hivi "Hata ukoo sina, sina ndugu wa damu. Wala kabila sina udini, sijui mmakonde!! Au msukuma, sijui mmasai au mluguru"
Kuna bridge ya kimchiriku Banza anaimba "Nalia lia mama oooh, uko wapi mama oooh, nalia lia mama ooh! Uko wapi mama oooh!! Nataka kucheza eeh nataka kudekaa!! Kucheza eeeh! Nataka kudekaaa!!"
Kama kuna mtu anao, au anaujua jina mnipatie niweze kuupata, wimbo unanikuna sana huu. Msaada wenu please wana JF
Naupenda sana ila kuusikia kwake kwa nadra sana!
Nilikuwa kwenye basi majuzi Radio moja hivi tukiwa Morogoro waliupiga!!
Niliwachokoza abiria wenzangu kuhusu uzuri wa huo wimbo lakini hakuna aliyeujua jina ingawa wengi waliupenda pia!! Na bahati mbaya mtangazaji hakuutaja jina wala mwimbaji so alituachia ubishi mkubwa sana kwenye basi!!
Mi nilijua alifanya kama featuring kumbe ni enzi hizo akiwa TOT!!
Thanks sana mkuu, uwe na Jumapili njema