Salim Ahmed Salim, yule Mpemba wa Mkoani asiye na makundi,nongwa wala visasi.
Mwepesi kusamehe na kusahau,msikivu na mchapa kazi.
Alikua last PM (of the URT)wa Mwalimu Julius Nyerere,
Akawa waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa(+naibu waziri mkuu wa JMT) chini ya Ali H.Mwinyi,
Baada ya hapo akaenda Addis Ababa kama katibu mkuu wa iliyokua OAU na alichapa kazi kama mwafrika mkereketwa.
Kabla ya hapo wengi wanajua historia yake iliyotukuka huko ughaibuni ila kubwa la kukumbukwa ni wakati akiwa mwakilishi wa kudumu umoja wa mataifa enzi za upiganiaji uhuru kusini mwa Afrika.
Salim alitoa mchango usioelezeka kwenye ukombozi wa Msumbiji,Zimbabwe(south rhodesia),Namibia,Angola,Capeverde,n.k, n.k.
Najua wengi humu JF ni wanaharakati,wanavyama vya siasa,wenye mirengo(leftists,rightists na centrists).
Ni wachache sana wako kiuzalendo zaidi.Hivyo natarajia michango iliyopindapinda na hasi kuhusu huyu bwana kubebeshwa jukumu la kuongoza hili Taifa.
Katika kipindi hiki cha mpito kuelekea kwenye kundi la BRICS taifa hili linamhitaji mtu kama Salim.
Sio Silaa,Mbowe,Lowasa,(or the other group of the sixes-Sita,Mwakyembe,Magufuli,etc),Membe,Nchimbi,Asha-Rose.
Wala halihitaji akina Shein,Seif,Hussein Mwinyi,Shamsi Vuai,n.k n.k.Halihitahi Mzanzibari,Mzanzibara,Mtanganyika,Mkaskazini,Mpwani,Mwanamke wala Kijana.Halihitaji ccm,cdm,cuf wala nccr..Linamhitaji MTANZANIA MZALENDO!!