Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Naibu Meya wa Jiji la Ilala Dougras Didas Massaburi ambaye anahusishwa na kugombea Jimbo jipya la Kivule endapo litagawanywa Jimbo la Ukonga, amesema na yeye ameona taarifa hizo mitandaoni, lakini kwa sasa nguvu amezielekeza kwenye uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Soma: Mchuano mkali katika jimbo jipya la Kivule. Naibu Meya Jiji la Ilala anatajwa huenda akajitosa kuwania Ubunge
"Nimeona tetesi nyingi zikinitaja lakini kwa sasa nipo mtaani nakimbizana na hizi siku mbili za mwisho za Daftari La Kudumu tumejipanga kutafuta kura nyingi za Raisi Dkt. Samia na Mwenza wake Dkt.Emmanuel ndio jambo mahususi kwa sasa na tayari tunaongoza kwa Ilala uandikishaji sasa umefikia watu 22,000 mpaka jana jioni kati ya wakazi 40,000 plus kwa mujibu wa sensa kwahiyo nitoe wito wananchi na wana CCM wenzangu waache habari hizi wajikite kumpa zawadi Rais kwa kazi kubwa aliyoifanya Ndani ya Jiji letu la Ilala yenye Majimbo matatu na wabunge watatu ambae ni Jerry Silaa, Bona na Zungu na tunaendelea kuwategemea kutuvusha tena uchaguzi ujao" - amejibu Massaburi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Chanika.