Nahitaji kufahamishwa

Optimistic_

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2017
Posts
2,347
Reaction score
1,860
Jamani kwema,

Naomba kujua tofauti ya Smart TV na LED TV?
 
Kwa ujuzi wangu

Smart tv vi tv flat za kisasa zaid zinazokuja na options yakisasa zaidi..... Ambazo ndani yake zinasoftware za kuweza kuingia kwenye mitandao ya kijamii ukiunganisha kwa wifi na sim yako ya mkononi yaan smart phone wakati
Led tv ni tv za kawaida (flat) ambazo hazina hizo option ya mitandao ya kijamii na kadhalika.

Yaani unaweza kuingiza signal zako za av au pc au HDMI. Lakini neno LED hilo linasimama kuonyesha aina ya kioo ambacho tv yako inatumia. Kwa hivyo smart tv ni led hata ambazo sio smart ni led pia. Wakati zile za chogo kioo chake kinajulikakana kama vfd.

Naimani kwa sehemu nimekuelewesha
 
LED TV ni runinga yeyote ile ambayo imewezeshwa kuwa na picha ang'avu kutokana na aina ya kioo (Display) ambacho ni LED. Yaani hutumia 'Light-Emitting Diodes' kama chanzo cha mwanga nyuma ya kioo cha runinga tofauti na mifumo ya runinga nyinginezo. Faida zake kuu ni;
  • Inapunguza matumizi ya umeme (Energy Efficient) ukilinganisha na LCD pamoja na CRT.
  • Picha ang'avu na bora zaidi (High Definition).
LED TV's ndizo runinga zenye gharama kubwa zaidi kutokana na faida zake ukilinganisha na runinga nyinginezo kama LCD n.k.

Smart TV ni runinga ya Kidigitali iliyowezeshwa kuwa na huduma ya Internet na moja ya faida zake kubwa ni uwezo wa kupata chaneli mbalimbali bila ya matumizi ya antena (Antenna, Satellite Dish, Cable). Haya ni maboresho ya kwenye runinga yanayoshabihiana na ya simu za mkononi kama vile 'Smartphones'.

Katika Smart TV unaweza kutazama 'Videos' ama vipindi vya runinga (Video Streaming) mitandaoni hususani katika mitandao kama vile Netfix n.k. Pia inakupa uwezo wa kuperuzi mitandaoni hususani mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter n.k. bila kusahau mitandao uhusuyo michezo ya runinga (Video Games). Hayo ni machache tu kati ya yale ambayo unaweza kuyafanya kwa kutumia Smart TV.

Utofauti:
Utofauti mkubwa kati ya LED TV na Smart TV umejikita zaidi kimuundo na utendaji kazi:

LED TVs zinakuwa na muundo wa 'Display' ama kioo cha LED na si vinginevyo lakini kwa upande wa Smart TVs ni katika utendaji kazi ila zinaweza kuwa katika miundo tofauti na LED. Yaani Smart TV haina mahusiano yeyote yale na haifungamanishwi na kioo cha runinga husika.
 
Nimekupata vizuri mkuu....

Asante sana...


Na nyingne nimeona zinaandikwa normol flat tv hizi nazo zina toafuti gan na LED au smart??
 
Nimekupata vizuri mkuu....

Asante sana...

Na nyingne nimeona zinaandikwa normol flat tv hizi nazo zina toafuti gan na LED au smart??


Pia naomba kujua faida za FLAT CURVED TV ukilinganisha na FLAT TV kawaida
 
Kuna mahali umeandika kwamba LED TV ina gharama zaidi...

Mbona naona Smart ndo ni ghali zaidi kuliko LED
 
Nimekupata vizuri mkuu....

Asante sana...

Na nyingne nimeona zinaandikwa normol flat tv hizi nazo zina toafuti gan na LED au smart??


Pia naomba kujua faida za FLAT CURVED TV ukilinganisha na FLAT TV kawaida
Mkuu neno led lisikuchanganye
Tv zinavioo tofauti hicho led kama alivosema mkuu vinatumia umeme mchache pia picha yake ni angavu inaonekana vizur
ila vioo vya vfd hivi havina picha nzuri oia hutumia umeme mwingi
Hivyo smart tv ni LED Na ambazo sio smart ni Led pia ila zote flat
 
Nina samsung hapa inches 50 ni imeandikwa LCD PLASMA huku nyuma enyewe ni 296watts sasa hii ndo vipi namaanisha kiubora, Pia ni kwamba zipo tv ambazo ni 50 inches kama hii ambazo ni LED tv zenye watts ndogo zaidi.. auu
 
Kwa lugha nyepesi, ni kwamba Smart TV ni televisheni inayoweza kuunganishwa na internet.

Hivyo basi huwa inaambatanishwa "software" ndogo ndogo tofauti ziitwazo "apps" au "applications" zenye kukuwezesha kufikia "access" vitu mbalimbali kulingana na matumizi ya app husika.

LED au LCD au Plasma TV kwa lugha nyepesi majina hayo yametoka tu na muundo wa kioo cha televisheni, ni teknolojia tofauti.Moja hutumia diodes, nyingine liquid crystal, nyingine gas iliyokuwa ionized.

Hivyo basi Smart TV, mtu mwingine anaweza akaiita LED Smart TV, ama LCD Smart, ama 4k Smart TV n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ