Mbona hela ndogo sana hiyo jiongeze kidogo maana hicho kiasi ni kidogo sana kwa kweli. Imagine kukodi taxi toka Ubungo hadi posta ni 20,000 na mtu anatumia saa moja tu analiachia gari, sasa wewe unachukua Noah na dereva kuanzia asubuhi mpk kesho yake saa 12 jioni ina maanisha hata ukulitumia kubeba abiria buku mbili mbili unapata faida hata mara tatu.
Nachojua Noah ukiikodi kwenye harusi pamoja na dereva ni 100,000 tu
Pia kwa hiyo bei ina maana kwa siku unakodi kwa 25,000 dereva sijui atalipwa ngapi kwa siku chenji ibaki tajiri nae apelekewe chake
Hebu jiongeze kwa mchanganuo niliokupa hiyo deal hailipi kabisa bora hata ulipaki Noah uwe unaliangalia tu kuliko kulichakaza siku 2 kwa fifte