Jamani mbona basi wanahofu kubwa hivyo?nkomelo miomgoni mwa matatizo yanayo mfanya atendewe hayo ni;
1. Anaonekana akigombea 2015 chama kinaweza pata ugumu sana katika kushinda uchaguzi maana anadoa tayari.
2. Lowasa anaonekana anauwezo wa pesa kuliko wagombea wengine ndio maana wanamchukia.
3. Lowasa anahisiwa kuwa akishinda uchaguzi atakuwa na mtu wa kisasi(kumbuka sababu na chamzo cha kutolewa kwenye uwaziri).
4. Lowasa amekuwa na kiburi na dharau sana hata kwa viongozi wake wa chama.
5. Yale maneno ambayo watu wanayatukuza sanaaaaa ya aliyekuwa raisi wetu wa kwanza.
Acha wamzushie tu kama Zuma au Uhuru Kenyata... Wanamkandamiza wakati wanajua chama kizima Lowasa pekee ndiye wa kuipiga mweleka cdm
Acha wamzushie tu kama Zuma au Uhuru Kenyata... Wanamkandamiza wakati wanajua chama kizima Lowasa pekee ndiye wa kuipiga mweleka cdm
nkomelo suala sio hofu, makundi yote ambayo yako dhidi yake wanajua akishinda urais lazima alipe kisasi na inawezekana alishamtamkia jk ndio maana jk amewahi kusema kuwa kuna watu wengine ni watu wa visasi kwa hiyo hawafai kuwa maraisi wa nchi yetu.
Lowasa hana jeuri ya kuipiga mweleka cdm! Ni mtumba tu tena uliochoka sana!
Lowasa ni mgonjwa jamani, mwacheni apumzike!
MSALANI, hata mimi nashangaa sana uvumi wa watu. Kuna watu humu wanajifanya wanaijua afya ya Mh.Lowasa kuliko yeye mwenyewe na mke wake. Sasa sijui ndiyo tuseme wapo karibu naye zaidi kuliko mke wake???Lowassa asema yuko fiti kwa lolote. - YouTube
Kwenye hiyo video, mke wake anasema yuko fit, hana shida yeyote, wewe kama unajua ni mgonjwa tueleze ugonjwa wake, maana unaonekana uko karibu na Lowassa kuliko hata mke wake!
Ya el kama ya zzk; kumtia kabali/ngwara mgombea tishio kabla ya kufika mbele ya sanduku la kura. Huo ni ufedhuli katika demokrasiaNimekua ni kifuatilia mbio za u rais ndani ya ccm. Nimekuja kubaini mzee Lowasa anaonewa sana na baadhi ya viongozi wa chama.
Anatupiwa lawama Eti ameanza kampeni kabla ya wakati; Eti anatumia makanisa na misikiti kuusaka u rais na kwamba anatumia fedha katika harakati hizo.
Kinachonisumbua kwanini yeye tu?
Mbona Mzee Sitta, Sumaye, Makamba nk nao tumewaona makanisani wakifanya shughuli kama anazofanya mzee Lowasa huko ila kwao viongozi wa chama wanaona sawa tu.
Eti kaanza kampeni mapema ina maana kweli chama hawajui Wasira, Membe, Ngeleja, Makamba Sitta nk wao wanachofanya ni nini? Wao hawasemwi kwanini?
Kuhusu matumizi ya Fedha mbona tumesikia wote niliowataja hapo juu wakituma salaam zinazoambatana na mapesa Kwa wajumbe wa ccm.
Ningefurahi kama chama kinataka kushughulika na hili kiwe fair enough Kwa wote isiwe Kwa Lowasa tu! Wanaotoa matamko nitawaheshimu Iwapo watakua wakweli Kwa watanzania Kwa kueleza bayana wapo wengi wameanza kampeni mapema, wanatumia makanisa/misikiti na wanatumia fedha sana tu.
Vinginevyo Lowasa anaonewa!