Nafasi ya mwanamke katika Jamii

Skillzkid_

New Member
Joined
Aug 14, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Bi Rachel Chebet Ruto ni mke wa Rais aliyeshinda nafasi ya kiti cha Urais nchini Kenya, ni mwanamke kinara mwenye upendo, elimu na mwanaharakati za kuwainua wanawake kiuchumi.

Ushupavu wake umesaidia kuleta mabadiliko ya kifikra chanya kwa wanawake wengi wa Kenya, amejitahidi kuwashika mkono vijana, wazee na wanawake kwa kuwaongoza na kuwasaidia katika hali zao za kimaisha.

Harakati zake zimefanya awe na mawazo tofauti ya faida. Mradi wa maji ambao umesaidia wanawake kutotembea umbali mrefu kutafuta maji, mradi wa kushona vitambaa kwa wafungwa wanawake ili pesa inayopatikana iwasaidie wakitoka magerezani na mradi mkubwa ambao wanawake wengi wanaufahamu wa Table Banking unaowakutanisha wanawake ambao ni washiriki kuchangia fedha kila baada ya muda fulani na kuweza kufanyia shughuli mbalimbali.

Kutokana na maisha ya Bi Rachel Ruto kuna mengi ya kujifunza kwa wanawake wapambanaji na wenye maono ya kufika mbali kwa kuendelea kuwashika wengine.

 
WAMEKUSIKA MKUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…