J e huyo ndio mpenzi wako wa kwanza?? Je kwani kila uhusiano baina ya mvulana na msichana uwe ndoa??? Kwani umeambiwa na mganga ya kwamba ukioana na huyo mchumba utakuwa tajiri?? Kwani umepata hasara ya shilingi ngapi kwa kumwacha?? Jaribu kutulia na kujibu hayo maswali, kisha utaona kama unayo sababu ya msingi ya kuchukia mapenzi.