Kwenye jimbo la Siha, tukiachana na vichekesho vya Mh Mwanri, hakubaliki kabisa jimboni.
Alipokuwa Naibu Waziri TAMISEMI,alijikita zaidi kwenye mambo ya kiserikali. Na kusahau kabisa uwakilishi. Kujiamini kulikopitiliza pamoja na Upepo wa Lowassa ukamuangusha.
Atakayepita itategemeana na busara za kamati kuu. Kama Mwanri alishauriwa agombee na WAKUU, basi atapita. Kama ni utashi binafsi, hana chake.
Siha mpaka sasa wamejitokeza watia nia zaidi ya watano. Ila mpute mpute upo baina ya hao wawili.