Mwenyekiti wetu wa Kamati ya bunge ya Mambo ya nje uko wapi? Mbona kimya toka ulipotoka Nigeria? Huku nyuma wenzio tumetishiwa nyau na Cameron kwamba fedha zake haziliki mpaka tuhalalishe mapenzi ya jinsia moja. Waziri wa Mambo ya Nje kaongea na kukataa fedha zinazonuka dhambi ya kudhalilisha utu wa mwafrika. Sasa tukiwa tunasubiri kauli yako, muda umezidi kusonga na ndipo nikajiuliza, wewe na kamati yako mko wapi katika hili? Unaliunga mkono au mna kigugumizi kama wenzetu ambao wameshikwa na kigugumizi kwa sababu ya nasaba ya chama chao na Cameron na chama chale cha kihafidhina? Mwenyekiti ongea kitu kama ulivyofanya kwa suala la Misri na Algeria. Ongea Mwenyekiti!