JUSTIN MPOTWA
Member
- Jan 16, 2013
- 16
- 11
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.Willbrod Slaa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa kimepanga kujenga mnara wa kumbukumbu katika kijiji cha Nyololo ili kumuenzi aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, aliyeuwawa katika kijiji hicho.
Mwangosi aliuwawa katika kijiji hicho Septemba 2, mwaka jana kwa kulipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa bomu baada ya kutokea vurugu kati ya wafuasi wa CHADEMA na polisi.
Katibu wa CHADEMA jimbo la MufindiKusini, Emmanuel Ngwalanje, akizungumza na NIPASHE jana alisema mnara huo ambao utagharimu kiasi cha Sh. 3,500,000 utaanza kujengwa Agosti 20 na kukamilika Agosti 28, mwaka huu na kuwaomba wadau kusaidia fedha kufanikisha ujenzi huo.
Ngwalanje alisema mmiliki wa eneoalipouwawa Mwangosi amekubali kutoa kibali cha kujengwa mnara huo, hivyo baada ya ujenzi kukamilika Septemba 2, mwaka huuambayo ni siku aliyouwawa, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.Willbrod Slaa,ataweka jiwe la msingi na kuzungumza na wananchi.
Alisema siku hiyo pia kutafanyika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia mjane wa Mwangosi na watoto wake.
Katibu huyo aliwataka wadau kusaidia kuchangia gharama za ujenzi wa mnara huo ili ujenzi uanzeharaka na kukamilika kwa wakati.
Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, anadaiwa kuwawa wakati polisi walipofyatua mabomu wakati CHADEMA wakiwa katika harakati zakufungua tawi la chama hicho katika kijiji cha Nyololo.
Kabla ya kuuawa kwa mwanahabarihuyo, mabomu yalipigwa eneo hilo ili kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisiyao.
CHANZO: NIPASHE
Pamoja sana Makamanda, Mungu awatangulie katika shughuli hiyo nzito ila damu ya Mwangisi iwe ni chachu ya ccm kulaaniwa na wale ambao bado wana i support.asante kwa taarifa , ntaleta mchango bila shaka .
Khaa ivi mwangosi alikuwa na harakati gani za kuikomboa tz?
acheni kujaza watu ujinga banasiku moja utajua tu.