Mwanaume ni macho,,Mwanamke ni maneno!

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,193
^^
Chanzo cha asili na ambacho huwafanya mwanaume na mwanamke wavutike katika mapenzi kabla ya mambo mengine ni kama ifuatavyo.
...
Mwandishi wa kitabu cha 'The act of marriage ' Tim Lahaye na mkewe Beverly wanabainisha kuwa "..Mwanaume hudanganywa na macho,Mwanamke hudanganywa na maneno.."
..
Mwanaume matamanio ya mapenzi yapo katika macho.Huweza kuvutiwa na umbile la mwanamke,matiti,paja, nywele,mwondoko au chochote ambacho kinaonekana kwa macho.
Mafundi wa wamitindo ya mavazi ya wanawake,viwanda na wengineo wanajua siri hii na ndio maana kila uchao wanaibuka na mitindo mingi ambayo kwa makusudi tu ni kuyaacha wazi maumbo yalitakiwa kusitiriwa,yawavutie wanaume.
..
Mwanamke huvutwa sana na maneno. Wanaume walio mafundi wa kudalizi maneno mbele ya wanawake,huwanasa kwa urahisi sana wanawake walio wengi. Si mara chache utawasikia wanawake wakisema 'sauti yake hunifanya nijisikie moto'.
Mpangilio wa maneno,ahadi tamu,na imaginary world ni anguko la wanawake wengi.
..
Hapa jamiiforum,wanawake wenye avatar zenye mvuto sana,watakuwa mashahidi jinsi profile zao zilivo na visitors wengi wanaume,,na kwa kuwa Jamiiforum inazidi kukua pengine wanawake watawekewa audio JF,waache kufaidi tu maneno ya maandishi toka kwa wanaume waliojaliwa ulimi wenye chemichemi ya asali
^^
 
mwandishi huyo kasema ukweli. nampenda sana Lahaye! kupitia kitabu chake cha 'I Love You But We are different', nilijifunza kutokuchukia mume wangu anapopenda sana mpira na kusahau kuwa nipo!
 
Enzi zetu sisi ulikuwa ukimbananisha mlimbwende engo thita hachomoki hata kwa dawa...
Basi utapata mtoto kang'ata kidole cha mwisho anasikiliza tu kidume unavyomwaga ngonjera zenye urali wa vina...
Kama kulikuwa na kichaka cha mti pembeni, ukishaona mti mzima umenyofolewa majani yote basi ujue hapo somo limeeleweka...
Au kulikuwa na jibu moja hivi, mlimbwende akikuambia kuwa, "basi nipe muda nifikirie"...yaani huo ulikuwa tayari ni ushindi wa mezani, bado tu kupewa kombe...
Sina uhakika kama vijana wa siku hizi bado wanajua kutema maneno ya kuchokora penzi la mwanamke...
 

^^
Ha ha ha Ngoja niwaite hawa watuambie kama wameona rafiki zao waking'ata vidole kupitia simu au live!
Lady doctor Heaven on earth Smile Ablessed christine ibrahim Nivea Passion Lady madameA Madame B na wengineo
^^
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:

lakini Himidini siku hizi nasikia
dunia imezunguluka,wadada wanapend
mahela na magari mazuri,maneno hayana tija
enzi zetu ndio tulikamatwa na maneno!!
 
Last edited by a moderator:
rabeka....Himidini ni kwel!
Ila dah,kiukweli hizi fasheni ni noma!
Ila,ukiacha mambo mengine(other things remain constant) mbona mi pia navutiwa na muonekano jamani,km wanaume!?
Au mi nina matatizo?
..halafu ckuhizi maneno sio sanaaa
 
Ha ha ha haya ngoja na mimi niweke picha ya mwanamke mrembo:smile-big: we mwanaume umenikosha!
 
^^
Ha ha ha Ngoja niwaite hawa watuambie kama wameona rafiki zao waking'ata vidole kupitia simu au live!
Lady doctor Heaven on earth Smile Ablessed christine ibrahim Nivea Passion Lady madameA Madame B na wengineo
^^
Enzi zetu ni kweli wadada walikua wanafanya hivyo kung'ata vidole , kuangalia chini lkn siku hizi mambo yamebadilika . Wanataka pesa na sio maneno mazuri na ndio maana utaona vijana hawana huo utaalam wa maneno wao huenda moja kwa moja kwenye point . Zamani mdada ataitwa majina mengi mazuri na ya heshima , kwakweli mambo yamebadilika sana.
 
Hakuna kunyonya vidole wala,kula majan..digital"online",ufilipino,friend with benefit........?????
 
Mmekosea nyie Wanawake hela,Fedha,chapaa....money!!ingekua maneno kila mzaramo angekua anaopoa akina Kyln na akina Mengi wanapigwa chini

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ha ha ha haya ngoja na mimi niweke picha ya mwanamke mrembo:smile-big: we mwanaume umenikosha!

^^
Hebu jaribu mimi49 halafu tuone mabadiliko ndani ya mwezi,,usisahau kunistua ukiwa humu mitaa ya jf,,tuone iwapo ka utafiti katafanikiwa.
^^
 
Last edited by a moderator:
NI ukweli mtupu, God made it that way purposely make kama wote wangekuwa wanashawishika kwa namna moja kamwe hao watu wawili ambao wakiungana wanakuwa mmoja wasingekuwa mmoja bali wawili. Tatizo Dunia ya leo baadhi ya wanaume wanataka kugeuka kuwa kama wanawake na wanawake pia wanataka kuwa wanaume. NI HTARI.
 
Hizo zote ni ngonjera.... bila fweza, hela, pesa... money, petha! m/ke atakuangalia afu mwishowe utasikia mxiiiiiiiiiiii...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…