Kwa akili ya Werema huwa anamwangalia mtu na sio hoja, lakini kiti (mwanasheria mkuu)anachokalia kinataka kuangalia hoja, hivi kwa mantiki hiyo Werema anapishana na kiti chake anajitumikia yeye mwenyewe matakwa ya nafsi yake huku akila posho ya mwanasheria mkuu. Huu ni sawa na wizi.
Ndungai naye kama kawaida yake anamwangalia Lisu kama CHADEMA na anajiona yeye kama CCM. Lakini kiti anachokalia ni cha Bunge Tukufu la Jamhuri ya Tanzania. Nywele za Ndungai na Werema zinaonyesha jinsi wanavyofikiri tofauti na wanvyopaswa kufikiri ingawa wote wawili wana nywele.
Waingereza wana usemi wanasema 'Self qualification is no qualification' ikimaanisha sifa ya kujipa wewe mwenyewe haina thamani. Sasa tuwaangalie hawa watu watatu: Lisu, Ndungai na Werema, nani hajui kufikiri japokuwa anazo nywele? Nipeni jibu wana JF wekeni na supportings zenu bila biasness